Mrejesho: Manunuzi ya mtandaoni (ebay)

Mrejesho: Manunuzi ya mtandaoni (ebay)

Kuna watu wanakuwa na wasiwasi kwamba wanaweza kununua kitu then muuzaji aka-disappear baada ya kufanya malipo...
Hamna haja ya kuwa na wasiwasi kwani kwa mujibu wa policy ha paypal muuzaji anaweza kuchukua fedha zake baada ya siku 21 mara baada ya kufanya mauzo.. Na atapata fedha zake endapo tu hakutakuwa na malalamiko kutoka kwa mnunuaji.. Kawaida mzigo hadi kumfikia mteja unachukua siku 10 mpaka 20. So wana assumu kwamba ndani ya siku 21 tayari mnunuzi atakuwa amepata mzigo wake... So ni vyema kwa munuaji kumuulizia muuzaji kuhusu status ya mzigo wake baada ya siku nne.. Status ya mzigo wako unaweza ukaulizia au kwa kufanya tracking kwa kutumia aplication unayoweza download kwenye playstore..
Screenshot_2017-04-07-19-26-26.png
 
mkuu kna mzigo nimeagiza lakini natumia Aliexpress kwenye tracking unaonesha mzigo ushafika dodoma tangu juzi lakin cjapigiwa simu na watu wa posta vipi naweza kwenda posta kuclaim au nisubir mpaka nipigiwe simu?
Mkuu ulitumia Address gani kwa Dodoma, Pobox ya mkoa au una address yako bnafsi ?
 
Ukatumwa tarehe 16 na leo umefika..
NILICHOJIFUNZA
1. Wakati mwingine woga wetu ndio unaotufanya kuwa nyuma kimaendeleo.. Dunia ya sasa imekua kijiji unaweza pata bidhaa yeyote toka ulimwengu wowotena kwa bei rahisi cha msingi ni kutumia njia sahihi wakati wa manunuzi..
2. Wizi wa pesa kwenye acount.. Kuna wakati nilikua na wasi wasi kwamba uenda jamaa wangenipiga ela zangu kwenye acount.. Hii si kweli jamaa wa ebay wapo makini sana hasa hasa ukiwa na acount ya paypal yani chagua bidhaa ebay lakini lipa kwa kutumia paypal..
Kuna jamaa mmoja alikweka bidhaa kiwizi wizi nikainunua jamaa wa paypal walipogundua wakamblock jamaa na fedha zangu zikarudishwa kwenye acount yangu.. Haijalishi ni kiasi gani kitarudishwa..
View attachment 489334
KUHUSU ZIP CODE NA POSTAL CODE
Hizi zisiwasumbue.. Andika detail zako za nchi, mkoa na wilaya, na code yetu pendwa ya +255 plus jina lako kamili trust me mzigo wako utafikishwa posta kuu ya mkoa wako na watu wa posta watakupigia simu uufate mzigo wako mara unapofika.. Hasa wakituma kwa register.. Usiandike P. O. BOX kwani wengine huwa hawataki mtu atumie P. O. Box.
2. Kuna vingine vingi ambavyo ukiwa interested unaweza jifunza cha msingi tuache woga.
Naskia kuhusu akaunti kuibiwa pesa ni pale wajanja wa kuhack wanapotumia details zako kulipia bidhaa na kukomba zilizobak na si ebay wanaoziiba. Dawa ni kuwa na akaunt maalum ya malipo ya aina hiyo tu. Inabak haina kitu ukishalipia.
 
Naskia kuhusu akaunti kuibiwa pesa ni pale wajanja wa kuhack wanapotumia details zako kulipia bidhaa na kukomba zilizobak na si ebay wanaoziiba. Dawa ni kuwa na akaunt maalum ya malipo ya aina hiyo tu. Inabak haina kitu ukishalipia.
Ukifuata utaratbu hakuna anayeweza kufanya huo ujinga...
 
nikijisajili kwenye ebay,sasa nikifika kwenye comfermation ya mobile NAMBA inagona.nisaidie hapo wadau nifanyejee.
 
nikijisajili kwenye ebay,sasa nikifika kwenye comfermation ya mobile NAMBA inagona.nisaidie hapo wadau nifanyejee.
Ukishachagua nchi tayari inakua imwshaweka code number +255 so malizia zile namba zingine ukitoa/ ukiacha sifuri ya mwanzo.
 
je wakuu, kuna mitandao tofauti tofauti ya kuuza bidhaa,je kila mtandao inabidi nijisajili tena,au kwa kuwa nimeisajili paybal,basi ni rahisi nikiingia mkwenye mtandao wataweza kunipata na taarifa zangu zote,nitoeni ushamba hapo wadau
 
je wakuu, kuna mitandao tofauti tofauti ya kuuza bidhaa,je kila mtandao inabidi nijisajili tena,au kwa kuwa nimeisajili paybal,basi ni rahisi nikiingia mkwenye mtandao wataweza kunipata na taarifa zangu zote,nitoeni ushamba hapo wadau
Kama wana accept paypal tumia the same acount.. Tho kila mtandao una njia yake ya malipo.. Wengine hawa accept paypal
 
Kwenye manunuzi ya bidhaa kwa nji ya mnada (auction) kuwa makini coz waweza kuta bidhaa inauzwa usd0. 01 lakini shipping cost ni usd 98.
 
Back
Top Bottom