Mrejesho: Mke wangu anataka kuandika jina lake nyumba niliyoijenga

Huu ushauri usiufuate hata
Akikomaa tafuta uwanja mwingine kajenge.
Hiyo nyumba either muuze au ibomoe tu umuachie uwanja wake.
Ipo siku kaka zake watakuja wakufukuze hapo.
Watasema ni kwetu
Sisi ndio tulinunua huu uwanja
 
Hata mume siyo ndugu ila sasa mmejenga kwa ajili ya watoto...kwann mfarakane kwa vitu vya kupita mkuu
Watoto wanaweza ungana na mama kumfukuza baba.
Aafu ukute hata watoto kauziwa mbuzi kwenye gunia
 
[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]
 
Yaani mimi ni mwanamke, lakini mambo mengine yanafanya wanawake wote tuonekane tunajali mali kuliko ndoa. Mimi katika maisha yangu sitaki dhulma kabisa. Nina mwanaume nimenkuta ana watoto 2 , anajenga nyumba nikamuambia andika jina lako na watoto wako 2. Huyu mwingine wa kwangu ana mali zake ambazo ni zangu. Ikitokea la kutokea atarithi vyangu. Let's be fair kwenye haya maisha, mali ya dhulma haitakufikisha popote.
 
Acha tu sikujua hizo changamoto zingetokea. Ila hili limenivuruga kabisa. Yaani aliposema sema tuandike Majina yetu wote akapendekeza pia na kile kiwanja changu tufanye hivyo hivyo pia. Aise ni mtihani mkubwa.
Hahahah umeliwq kichwa. Pole sana. Ndio unajifunza sasq, hutafanya tena kosa hili hapo baadae.
 
Ushauri wako kisheria si sawa. Mkishaoana chochote kinachopatikana wakati mkiwa katika ndoa ni mali ya wanandoa. Hata hiyo nyumba kama imejengwa baada ya ndoa katika kiwanja cha mke inapaswa mume alipwe fidia ya nyumba iliyojengwa katika kipindi mpo ndoani

Mtoa mada fuatilia kuhusu sheria inasemaje na haki zako katika hiyo nyumba.
 
Najaribu kuwaza, siku mvurugane kisha muachane. Anaweza kukutimua wewe na Wanao kwenye hiyo nyumba kwa Kigezo kwamba ni Jukumu lako kuwapatia Urithi wanao, halafu yeye akaingiza mwanaume mwingine wakaendelea kuishi kwenye hiyo Nyumba...
😀😀😀😀. God dictates
 
Mwanamke hataki watoto waandikwe ili yeye akiwahi kufa ili ndugu zake wapate mgao (wazazi )
 
Mkuu mchako wa kutafuta pesa ni endelevu mpaka kifo inamaana bado upo upo
 
Hata mume siyo ndugu ila sasa mmejenga kwa ajili ya watoto...kwann mfarakane kwa vitu vya kupita mkuu
Nyumba ni kitu cha kupita???
Kiuchumi nyumba ni fixed. Siku ukiipita wewe na kuishia kutangatanga kulala kwenye penu za nyunba za watu au stand ndiyo utajua kumbe nyumba siyo kitu cha kupita
 
Nyumba ni kitu cha kupita???
Kiuchumi nyumba ni fixed. Siku ukiipita wewe na kuishia kutangatanga kulala kwenye penu za nyunba za watu au stand ndiyo utajua kumbe nyumba siyo kitu cha kupita
Vizuri
 
Kwanini msiandike majina yenu wote? Yaani watoto na wazazi? Hata wanaume huwa mna huo mchezo wa kudhulumu mali. Kwa mfano ukija kuoa mke mwengine, huyo uliejenga nae ataenda kukaa wapi wakati jina ni lako
 
Wanaume wengine bana! Unakuta mwanamke ana kiwanja yaan unaweka room mbili unataka uwe mmiliki? Unampora haki ya jasho lake? Kuna wanaume mlipewa hiyo jinsia kwa bahati mbaya kabisa! Khaaa nliolewa na mume wangu nikiwa nimeanza maisha yangu nikiwa na assets kadhaa nyumba na viwanja vikiwemo, nikwambie mwanaume wewe kuwa, haijawahi kutokea hata mume wangu akaongelea chochote kuhusu alichokikuta maana anajua hata asipomiliki yeye watoto wake ndo wamiliki! Na kuna vitu vingi amefanya juu ya hizo assets na hata haziongelei eti sjui amiliki nan, anachofanya ni kunishauri tuuu na anapitaga anaviangalia nyumba anaenda kwa wapangaji anasimamia yaan wanajua ndo mmiliki ila vyoote alivyonikuta navyo viko kwa majina yangu na alisaidia kupata hati hata haongelei khhhhaaaa namhurumia huyo mwanamke mwenzangu aisee
 

kwa nini msiandike majina yenu wote ikawa ni mali ambayo nu joint owned, numeshaona hati zenye majina mawili mke na mume
 
Tafuta kiwanja kingine jenga nyumba mpya...alafu rudi uza hiyo nyumba ya sasa....60% ya hela baki nayo yeye mpe 40%

Sent using Jamii Forums mobile app
 
1. Kwa kuwa, umekiri kwamba ninyi ni wanandoa (mmefunga ndoa), na,
2. Kwa kuwa, umekiri pia kwamba mna watoto wenu wa wawili ambao wamezaliwa ndani ya ndoa.
Hivyo Basi, suluhisho sahihi zaidi kuhusiana na hili suala lako ni:-
(I) AIDHA, Ardhi hiyo mnapaswa kuimiliki kwa pamoja nyinyi wote wawili kwa umiliki wa pamoja (Joint Occupation or by means of Occupation in Common.
(a) Mmiliki Ardhi hiyo wote kwa pamoja kwa umiliki wenye maslahi yasiyogawanyika, yaani Joint Tenants (Matrimonial Property).
Majina yenu wote wawili (jina lako na la huyo mwanamke) yawepo kwenye Hati ya Umiliki wa Ardhi, hii itaondoa utata na wasiwasi wa kudhulumiana hiyo Ardhi.
(b) Mmiliki Ardhi hiyo wote kwa pamoja kwa Hisa, yaani Common Occupiers in Shares. Mnaweza mkagawana Hisa za umiliki wa hiyo Ardhi, kila Mwanandoa anaweza akamiliki Ardhi hiyo kwa Hisa ya 50% au vinginevyo kwa kadiri mtakavyokubaliana ninyi wenyewe kwa hiyari yenu.

( ii) AU, Wote wawili, yaani wewe na mkeo mnaweza mkajitoa kwenye suala la Umiliki wa hiyo Ardhi, badala yake Ardhi hiyo muimilikishe kwa Watoto wenu na nyinyi mkabaki kuwa wasimamizi tu wa Ardhi husika (Guardianship) hadi hapo watoto wenu watakapofikia umri wa utu uzima wa miaka 18 au zaidi.

NB: Nimeshauri kulingana na uzoefu wangu binafsi wa kimataifa, yawezekana pengine ushauri wangu unakinzana na matakwa ya Sheria za Tanzania, Sina uhakika kuhusu suala hili lakini.
Lakini sehemu nyingi Sana ambazo nimewahi kuzuru, ushauri Kama huu umesaidia Sana katika kutatua Migogoro Kama huu wa kwako.
Naomba kuwasilisha.
I stand to be corrected!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…