Mrejesho,mtoto wangu wakiume umri miaka 10 anakojoa mkojo uliochanganyikana na damu

Mrejesho,mtoto wangu wakiume umri miaka 10 anakojoa mkojo uliochanganyikana na damu

Sasa majira ya saa nane alikunywa maji baadae saa moja kasoro akapata mkojo nikampa akakoje akapata mkojo usio kuwa umechanganyikana nadamu yaan alipata mkojo wa kawaida naambatanisha napicha,, Sasa
jibu liko hapa
 

Attachments

  • IMG_20260917_184540.jpg
    IMG_20260917_184540.jpg
    375.5 KB · Views: 7
Nakushauri Ndugu uende Hospital Kubwa, kama unaenda Hospital za Uchochoroni hutapata tiba, Fanya Mpang kama vipi Mpeleke Mtoto Muhimbili
Hii hospital nimeenda nihospital ya mkoa yaa hospital rufaa
 
Niko mkoani mbona nimemuhoji dokta mara mbili mbili narudia kumuuliza kichocho je anasema hana kichocho hakijaonekana kwenye vipimo
Pole sana atakuwa sawa.

Nilishaumwa kichocho miaka hiyo, kwa sasa tuliokulia Bushi. Madimbwi ya maji yalitusababishia kichocho sababu ya kuogelea.

Tulipona tu bila hata Dawa
 
Amepimwa Hadi hicho daktar akasema hana
Aseee pole mkuu!! Usisite kuchukua hatua ifikapo kesho lakini uwenda ni jereha tu kidgo njia ya mkojo.

Ila ni vema ukarudi hospital tofauti kwa uchunguzi zaid wa kitabibu.

Pole sana mkuu mtoto atakuwa Sawa tu Mungu mwema.
 
  • Thanks
Reactions: Cyb
Mnunulie madafu anywe kama 3 au zaidi kwa siku 3 ukiona tatizo bado lipo. Tafuta hospital kubwa(yenye vifaa vya kisasa) mpeleke mtaalamu atakupa majibu sahihi zaidi.
 
  • Thanks
Reactions: Cyb
Habar wakuu nimerudi kuwapa mrejesho,asubuh ya Leo nilifika hospital yamkoa tukafanya taratibu zote za kumuoona daktar,nikaandikiwa nimuone daktar wamkojo bas tukaingia kwa daktar nikajielezea hali ya mtoto ilivyoanza mpaka mda huo,dokta akauliza kama mtoto alipigwa eneo husika lasiri akasema hapana,ulidondoka akasema hapana hapana
Akamuliiza ulicheza sana mtoto akajibu hapana,akaulizwa maji anayotumia akiwa shule ni yakisima
Kwaiyo tukaandikwa vipimo akaenda kupima mkojo,na damu fbp,fb-electrophosesis,figo,
Majibu yalitoka dokta akasema hakuna shida yoyote mkojo uko sawa,damu Iko sawa hakuna kichocho,figo ziko sawa,fullblood picture Iko sawa,red blood cell haijatoka,nkamuuliza shida nini Sasa akasema labda infection kwenye kibofu au figo,Sasa kama itatokea Tena itabid mje tuangalie zaid kibofu kama kina shida,au figo,au kansa ya kibofu
Sasa majira ya saa nane alikunywa maji baadae saa moja kasoro akapata mkojo nikampa akakoje akapata mkojo usio kuwa umechanganyikana nadamu yaan alipata mkojo wa kawaida naambatanisha napicha,, Sasa tumepanda gari tukarud nyumbani tumefikaa saa tatu kasoro uku tukiwa na kopo la mkojo amabao aliukojoa ukiwa sawa tu hauna damu,kama dakika 20 baadae nikamwambia akaumwage kumbe alivyoumwaga akawa kakojoa Tena katika Hilo kopo akaniletea niuone mkojo ulivyo,kuiona ni mkojo umeochanganyikana nadamu kama kahahawia hivi au nyekundu flani iliopauka naambatanisha napicha yake hapa chini,Sasa saa Tano hii akajiskia kama mkojo umembana kaenda kukojoa na chupa akapata mkojo ulio sawa mchachee kama vifuniko vitatu hivi vya chupa ya maji
Ule mkojo aliokojoa saa tatu hii uliochanganyikana na damu nikauchukua nikiambatana na mtoto Hadi hospital nikafika mida ya saa nne usiku huu nikajielezea vyooote ila dokta akasema kwa saa hii huu mkojo umeshakaa mda mrefu tukiupima hautaweza kutupa majibu sahihini nivyema ukaja asubuh hata alfajiri pindi atakapokua kabanwa na mkojo njoo nae
Wadau madaktari na wasio madaktari changamoto hii ya kijana wangu yaweza kuwa nini hasa kina msumbua mtoto
Pole sana mzazi. Kwa hali ya mtoto kuonekana kuwa na damu kwenye mkojo mara kwa mara, ni jambo linalohitaji ufuatiliaji wa kitabibu, hata kama vipimo vya awali vimeonekana kuwa kawaida. Umefanya vizuri kumpeleka hospitali na kufuata maelekezo ya daktari. Ni vizuri kufanya vipimo vya mkojo mpya kama mlivyoelekezwa, ili daktari aweze kupata picha sahihi zaidi ya hali yake.

Wataalamu wa afya na wenye uzoefu katika hali kama hii, tunaomba mtusaidie kuelewa kwa lugha rahisi; hali kama hii inaweza kuhusishwa na sababu zipi, na ni dalili zipi ambazo mzazi anatakiwa kuzichukulia kama za dharura?
 
Badili hospitali, dokta huyo sijamuelewa kihivyo, wakati huo huo ucheki na mambo ya kiroho. Yaende kwa pamoja tena kwa spidi.

Ungekuwa karibu yangu, ningekupa maji ya upako au mafuta ya upako.

Nina uzoefu mmoja, kuna dogo wa miaka 12 wakati huo, alianza kuumwa kifua ghafla, anakohoa, baafae akaanza kukohoa, makohozi damu. Hospitali hawaoni tatiizo kubwa. Nikapigiwa simu, nikawaambia tatizo lishughulikiwe kiroho pia.

Siku ya pili asubuhi na mapemanwakashughulikia kiroho, ndani ya nusu saa tu, mtoto hakohoi wala makohozi ya damu hakuna.

Tatizo lenu shughulikia kimwili na kiroho kwa wakati mmoja. Siku hizi mambo yamebadiilika, wapo wanywa damu pia.
 
Mpeleke haraka usikae nae ndani, ana maumivu au? Waangalie Kidneys zake pia muhimu
 
Back
Top Bottom