Mrejesho,mtoto wangu wakiume umri miaka 10 anakojoa mkojo uliochanganyikana na damu

Sasa majira ya saa nane alikunywa maji baadae saa moja kasoro akapata mkojo nikampa akakoje akapata mkojo usio kuwa umechanganyikana nadamu yaan alipata mkojo wa kawaida naambatanisha napicha,, Sasa
jibu liko hapa
 
Nakushauri Ndugu uende Hospital Kubwa, kama unaenda Hospital za Uchochoroni hutapata tiba, Fanya Mpang kama vipi Mpeleke Mtoto Muhimbili
Hii hospital nimeenda nihospital ya mkoa yaa hospital rufaa
 
Mzazi usiogope ni masuala ya kawaida, mabadiliko ya Kimwili

Kama upo Dodoma mjini, mpeleke Ntyuka Hospital (DCMC).

Ni kichocho hicho, relax atakuwa sawa.
Niko mkoani mbona nimemuhoji dokta mara mbili mbili narudia kumuuliza kichocho je anasema hana kichocho hakijaonekana kwenye vipimo
 
Niko mkoani mbona nimemuhoji dokta mara mbili mbili narudia kumuuliza kichocho je anasema hana kichocho hakijaonekana kwenye vipimo
Pole sana atakuwa sawa.

Nilishaumwa kichocho miaka hiyo, kwa sasa tuliokulia Bushi. Madimbwi ya maji yalitusababishia kichocho sababu ya kuogelea.

Tulipona tu bila hata Dawa
 
Amepimwa Hadi hicho daktar akasema hana
Aseee pole mkuu!! Usisite kuchukua hatua ifikapo kesho lakini uwenda ni jereha tu kidgo njia ya mkojo.

Ila ni vema ukarudi hospital tofauti kwa uchunguzi zaid wa kitabibu.

Pole sana mkuu mtoto atakuwa Sawa tu Mungu mwema.
 
Reactions: Cyb
Mnunulie madafu anywe kama 3 au zaidi kwa siku 3 ukiona tatizo bado lipo. Tafuta hospital kubwa(yenye vifaa vya kisasa) mpeleke mtaalamu atakupa majibu sahihi zaidi.
 
Reactions: Cyb
Pole sana mzazi. Kwa hali ya mtoto kuonekana kuwa na damu kwenye mkojo mara kwa mara, ni jambo linalohitaji ufuatiliaji wa kitabibu, hata kama vipimo vya awali vimeonekana kuwa kawaida. Umefanya vizuri kumpeleka hospitali na kufuata maelekezo ya daktari. Ni vizuri kufanya vipimo vya mkojo mpya kama mlivyoelekezwa, ili daktari aweze kupata picha sahihi zaidi ya hali yake.

Wataalamu wa afya na wenye uzoefu katika hali kama hii, tunaomba mtusaidie kuelewa kwa lugha rahisi; hali kama hii inaweza kuhusishwa na sababu zipi, na ni dalili zipi ambazo mzazi anatakiwa kuzichukulia kama za dharura?
 
Badili hospitali, dokta huyo sijamuelewa kihivyo, wakati huo huo ucheki na mambo ya kiroho. Yaende kwa pamoja tena kwa spidi.

Ungekuwa karibu yangu, ningekupa maji ya upako au mafuta ya upako.

Nina uzoefu mmoja, kuna dogo wa miaka 12 wakati huo, alianza kuumwa kifua ghafla, anakohoa, baafae akaanza kukohoa, makohozi damu. Hospitali hawaoni tatiizo kubwa. Nikapigiwa simu, nikawaambia tatizo lishughulikiwe kiroho pia.

Siku ya pili asubuhi na mapemanwakashughulikia kiroho, ndani ya nusu saa tu, mtoto hakohoi wala makohozi ya damu hakuna.

Tatizo lenu shughulikia kimwili na kiroho kwa wakati mmoja. Siku hizi mambo yamebadiilika, wapo wanywa damu pia.
 
Mpeleke haraka usikae nae ndani, ana maumivu au? Waangalie Kidneys zake pia muhimu
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…