Kwanza nimshukuru Mungu kwa kunipa afya tele, wakuu niingie kwenye mada moja kwa moja tarehe 6 mwenzi 12 mwaka jana niliomba ushauri nifanye nini niweze kuongeza kipato changu.
Kwenye ule uzi nilieleza mambo mengi sana nashukuru na watu walinishauri vizuri sana baada ya ushauri wenu nilianza kwanza kuwa na nidhamu ya pesa kwa kweli nimefanikiwa paka leo nimepata 200,000.
Sasa hii pesa natamani nikapange ili niweze kuhama pale kwa bosi wangu ila naona kama nikipanga na kuhama pale kwa bosi wangu siyo uwamuzi mzuri sana sasa wakuu naomba msaada wenu kwa hii 200,000.
Nifanye biashara gani ambayo ata kwa siku niweze kupata faida ata 5000 tu ambayo paka mwenzi hata wa tatu niwe nimeongeza kitu kidogo ili siku nikiwa taka kuondoka kwa bosi wangu niwe na mwanga wa kutosha.
Nitashukuru kama mtanipa ushauri mwengine