Mrejesho: Nataka Kumuacha, sina pa kuanzia

Nimewahi kupitia yanayoshabihiana na yako, kama kuna kosa ambalo mwanaume hapaswi kulifanya ni kumsahameme mwanamke mshenzi, hapa hata mimi niliwahi kukosea sana.

Samehe, ondoa kila kitu kwenye circle yako ambacho kinatafanya umkumbuke na kumtafakari.

Usije jaribu msamehe tena huyo mwanamke hata kama akatoa machozi ya kujaza ndoo ya maji.
 
Ilikuaje mkuu.
 
Ndivyo wanaume waaminifu wanayoyapitia, sometimes unawaza kuwa mpigaji tu na muhuni ila si kushauri uwe hivyo maana baya halilipizwi kwa baya bali kwa wema, wanawake wengi wanachukulia wanaume wapole na waaminifu kama mazoba ila sio haiko hivyo wengi ni wastaarabu na wamepata makuzi mazuri.
 
Unapo mpa nafasi na kusamehe pale unakua upo mafunzoni maana awali haikua rahisi kumuacha ila sasa unapokua na majuto mengi unakua na maamuzi ya kutorudi nyuma kabisa, maamuzi magumu yanataka sacrifice
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…