Mrejesho: Ni baada ya kupatiwa matibabu dhidi ya ugonjwa ulionikumba ghafla hadi kupelekea kulazwa hospitalini kwa siku mbili(2)

IamBrianLeeSnr

JF-Expert Member
Joined
Nov 10, 2022
Posts
2,010
Reaction score
4,179
Habari Wanajamii...

Ninatumai wote ni wazima wa afya kabisa pasina shaka, Mimi pia ni mzima na buheri wa afya kwa wastani wake. Kwa sababu bado naendelea na dawa kadhaa ili kuurudishia mwili afya tena kama ilivyokuwa hapo awali.

Naomba nianze na shukrani zangu za dhati kwenu wanajamii wenzangu mliokua na mimi sambamba kwa kunipa pole na faraja nyingi wakati nilipokuwa hoi hospitali, Niseme tu sina kitu cha kurudisha kama sehemu ya fadhila mliyoionyesha kwangu, Kwa sababu nilifarijika sana sana hata kuomba mungu azidi kuwaongezea baraka ktk utafutaji wenu na familia zenu zizungukwe na amani na utukufu wake daima.

Niweke hili wazi nilipitia mateso makali na magumu ambayo siku wahi kuyapitia katika nyakati yoyote ile ila kwa huu ugonjwa nilipata mfadhahiko mkubwa sana, Hata kuomba na kutubu makosa yangu yote nisamehewe, Niliowakosea wanisamehe na walionikosea niliwasamehe wote, Kusema ukweli nilifikiria sana na kujiuliza kuwa hii ndio safari imeisha au ni mtihani gani nimepangiwa kuupitia wakati huu, Sababu nilishiwa nguvu kabisa na kushindwa kufanya kitu chochote kama ilivyokuwa kawaida yangu.

353E1EC9-DAA7-42E2-A555-456B2675C969.jpeg

Namshukuru mungu kwa kuniinua tena na kuendelea na shughuli zangu kama nifanyavyo siku zote, Na leo hii nipo hapa kutoa shukrani zangu sana kwa hawa wanajamii walionyesha kujali kwa kuniombea na kunifariji kwa maongezi yaliyonipa nguvu na ujasiri wa kuamka tena...

SHUKRANI ZANGU ZA DHATI ZIFIKE KWENU:
Kennedy , USM ALGER , Unique Flower , mshamba_hachekwi , chrstopher , Nkundwe Sr , Mkanganyiko kukanganya , adden Fall Army Worm , Gily , Bei Elekezi , stephot Mamndenyi Wakuperuzi Asalamaleko Dalmine Troublemaker , Mickbrown , Numbisa , Smart Contract , Herbalist Dr MziziMkavu , OLUKUNDO , Uboboh , DR SANTOS , Prince Kunta , Mzee wa kupambania , kiboboso , Mpaji Mungu , Wrevta , Mamlukii , Palina , Akhi , Stroke , Cute Wife , Msanii , Depal , _Flames , DR HAYA LAND , Mpemba Mimi , Mr Devil , Katkit , Ushimen , Sharamdala , cocastic , Half american , amadala , Aaliyyah , Frank I Ritte , rikiboy , Smart Guy , Demi & Joanah

Licha ya kwamba sijatengamaa sawasawa kiafya ila nimependezwa na kutoa shukrani zangu kwenu na Kuwajuza kuwa hali yangu sasa inaendelea vizuri sana na hii yote ni kutokana na maombi yenu na neema zake mungu, Na mimi nawaombea mwendelee kupokea baraka za mungu milele kwani pasipo yeye hakuna awezae zaidi.

Ahsante...
 
Get well soon brother, tunafurahi umeweza kuandika Ata thread Imani yangu ni kwamba unaendelea vema na utarudi katika majukumu yako ya kawaida as soon as possible.

Hao members uliowataja hapo ni watu poa sana na ndo jamii forums yenyewe japo wapo wengi sana🤝🤝 very smart open minded nice guys and charismatic fellas.
 
Thank you brother 💪
 
Habari Wanajamii...

Ninatumai wote ni wazima wa afya kabisa pasina shaka, Mimi pia ni mzima na buheri wa afya kwa wastani wake. Kwa sababu bado naendelea na dawa kadhaa ili kuurudishia mwili afya tena kama ilivyokuwa hapo awali.

Naomba nianze na shukrani zangu za dhati kwenu wanajamii wenzangu mliokua na mimi sambamba kwa kunipa pole na faraja nyingi wakati nilipokuwa hoi hospitali, Niseme tu sina kitu cha kurudisha kama sehemu ya fadhila mliyoionyesha kwangu, Kwa sababu nilifarijika sana sana hata kuomba mungu azidi kuwaongezea baraka ktk utafutaji wenu na familia zenu zizungukwe na amani na utukufu wake daima.

Niweke hili wazi nilipitia mateso makali na magumu ambayo siku wahi kuyapitia katika nyakati yoyote ile ila kwa huu ugonjwa nilipata mfadhahiko mkubwa sana, Hata kuomba na kutubu makosa yangu yote nisamehewe, Niliowakosea wanisamehe na walionikosea niliwasamehe wote, Kusema ukweli nilifikiria sana na kujiuliza kuwa hii ndio safari imeisha au ni mtihani gani nimepangiwa kuupitia wakati huu, Sababu nilishiwa nguvu kabisa na kushindwa kufanya kitu chochote kama ilivyokuwa kawaida yangu.

View attachment 2639124
Namshukuru mungu kwa kuniinua tena na kuendelea na shughuli zangu kama nifanyavyo siku zote, Na leo hii nipo hapa kutoa shukrani zangu sana kwa hawa wanajamii walionyesha kujali kwa kuniombea na kunifariji kwa maongezi yaliyonipa nguvu na ujasiri wa kuamka tena...

SHUKRANI ZANGU ZA DHATI ZIFIKE KWENU:
Kennedy , USM ALGER , Unique Flower , mshamba_hachekwi , chrstopher , Nkundwe Sr , Mkanganyiko kukanganya , adden Fall Army Worm , Gily , Bei Elekezi , stephot Mamndenyi Wakuperuzi Asalamaleko Dalmine Troublemaker , Mickbrown , Numbisa , Smart Contract , Herbalist Dr MziziMkavu , OLUKUNDO , Uboboh , DR SANTOS , Prince Kunta , Mzee wa kupambania , kiboboso , Mpaji Mungu , Wrevta , Mamlukii , Palina , Akhi , Stroke , Cute Wife , Msanii , Depal , _Flames , DR HAYA LAND , Mpemba Mimi , Mr Devil , Katkit , Ushimen , Sharamdala , cocastic , Half american , amadala , Aaliyyah , Frank I Ritte , rikiboy , Smart Guy & Joanah

Licha ya kwamba sijatengamaa sawasawa kiafya ila nimependezwa na kutoa shukrani zangu kwenu na Kuwajuza kuwa hali yangu sasa inaendelea vizuri sana na hii yote ni kutokana na maombi yenu na neema zake mungu, Na mimi nawaombea mwendelee kupokea baraka za mungu milele kwani pasipo yeye hakuna awezae zaidi.

Ahsante...
Mungu azidi kukufanyia wepesi Mkuu, urudi kama zamani 🤲🏼
 
Back
Top Bottom