Mrejesho: Nilifanya biashara kwa wazo la hapa JamiiForums

political Engineer 2

JF-Expert Member
Joined
Oct 9, 2014
Posts
295
Reaction score
792
Mimi ni miongoni mwa watu wanaojaribu vitu vingi sana, Naamini katika so called risk taking.

Kuna mwana Jamii Forums humu alikuja na wazo, nilipoliangalia nikaona kama linawork, nikampigia simu akanipa ushirikiano nzuri sana( hakuwa tapeli kabisa nashuhudia hili hapa wazi wazi, he was a humble youth).

Biashara yenyewe ilikuwa ifanyike mkoani, sitaki kuitaja Kwa sababu mpaka sasa hata yeye hajui ID yangu hapa Jamii Forums.

Nilisafiri tukaanza biashara tulifanya vyema kama inavyotakiwa ingawa Niko busy sana nilikuwa namuachia.

Kwa ufupi niliingiza TSH 2,850,000 mpaka mwisho wa project nikipata jumla 520,000. Nilikula hasara kubwa mno.

Faida niliyopata ni shule, nikipata shule kubwa yapo mambo sitarudia kufanya, lakini yapo nitarudia kufanya ila Kwa umakini mkubwa sana.

Huyu kijana hakunitapeli ila tu basi biashara isikie hivi hivi, inalipa ikiwa inaadithiwa, ukiibgia ground unakutana na mengine kabisa ambayo hayakuwa kwenye hadithi.

Kama kuna mwingine ana wazi analodhani linaweza kutulipa vizuri karibu.
 
Funguka basi,mbona Zumaridi kafunguka wazi kasema yeye ni Mungu
 
Naomba nije pm Mkuu
 
karibuni HUDUMA YA KUHAMA, mtaa kwa mtaa na Dar kwenda mkoani.
Huduma zetu ni pamoja na;
[emoji117]kufunga na kufungua vitu tunapofika unapohamia
[emoji117]kupanga vitu mahala pake
[emoji117]kuweka mapazia na dish kama lipo
[emoji117]kukodisha gari la mizigo yako kama ukihitaji
[emoji117]kusafirisha mizigo mkoani

tupigie au watsapp 0685085466, tunapatikana kinyerezi DAR ES SALAAM
 
Kaka karibu katika biashara ya mchele
 
Biashara yenyewe ilikuwa ifanyike mkoani, sitaki kuitaja Kwa sababu mpaka sasa yeye hajui ID yangu hapa Jamii Forums.
Usiseme mpaka sasa huyo kijana haijui ID yako hapa JF wakati wazo ulilichukulia JF na huyo kijana ni wa JF na hii thd ipo JF,ina maana huyo kijana kama kaisha isoma hii thd,bado tu atakua haijui ID yako!
 
Sasa hizi ndio feedback zakuweka hapa. Tunaelezana ukweli wenyewe.
Hongera kwa kuthubutu mzeya. Sie wengine ata biashara ya bodaboda tunaogopa. Hela zimekaa tuu hazina la kufanya
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…