MREJESHO: Niliomba ushauri juu ya sehemu sahihi ya kutoa fungu la kumi

Baada ya kuomba ushauri hapa jukwaani, watu walichangia kwa hekima, kuna waliosisitiza nikatoe mahala ninapoabudu pia kuna walionishauri nikatoe kwa watu wenye uhitaji.

Pia kunawaliosema nikatoe ninapoabudu halafu pia nikatoe kwa wahitaji.

WOTE MLIOCHANGIA, NAWASHUKURU SANA.

Mm na mke wangu tulionelea tukatoe kwenye kituo cha yatima.

Si kwamba hatuheshimu madhabahu, Ni kwamba uwezo wetu kwa sasa ni duni hatuwezi kumudu kutoa sehemu zote mbili.

Hata huko kwa yatima tulikoenda tulienda kwa aibu, maana tulichonacho nikidogo mno.

Ila mkipata nafasi nendeni mkawaone hao watoto, maana kwa mujibu wa alietupokea ni kwamba several times wanalia uji.

Ni hayo tu.
ITOSHE KUSEMA AHSANTE KWA USHIRIKIANO
Ni jambo jema ulilofanya lakini hiyo sio zaka ni sadaka nyingine tu. Zaka inatolewa madhabahuni. Lengo la zaka ni kuendeleza huduma. Kwa mantiki hiyo utapata baraka za utoaji lakini hutapata baraka za zaka kama ambavyo ziliainishwa kwenye kitabu cha Malaki. Ukitaka baraka za kutoa zaka toa zaka madhabahuni.
 
Hongera sana kwa hilo mdau,ni jambo jema na la heri but!

Nakumbuka ktk uzi wako huo wapo walioku-challenge kwamba “unatoka nje ya familia/ukoo wako kwenda kusaidia kwengine (sisemi ni jambo baya au umekosea lah) vipi ktk circle yako hukuwa na ndugu anayehitaji huo msaada?hakuna yatima yeyote ktk ukoo wenu,je hapo jirani labda?”

Nb;sina lengo la kumkosoa mleta mada najaribu kujifunza kitu hapa
Nimejifunza kitu hapa na kimenigusa Sana mpaka chozi limetaka kunitoka , ulivyosema hakuna ndugu au majirani wenye shida, na kwa kipindi hiki Hali ngumu Sana hasa vijijini, na hata baadhi ya jirani zetu, watu wanakatiwa maji wengi mitaani ndo hapo kujiuliza Maisha yamekuwa sio Kama zamani.
 
Yani unaenda kumpa mtu hela akanunue V8 au akajenge Hotel halafu unaona umetoa sadaka wakati kuna maelfu hawana hata chakula.
Na hao ndiyo wanaharibu GDP ya nchi maana uwiano wa nguvu kazi iliyopo na kipato cha mtu mmojammoja haviwiani kutokana na wahuni wasiotoka jasho kuvuna zaidi kuliko wanaotoil mashambani
 
Baada ya kuomba ushauri hapa jukwaani, watu walichangia kwa hekima, kuna waliosisitiza nikatoe mahala ninapoabudu pia kuna walionishauri nikatoe kwa watu wenye uhitaji.

Pia kunawaliosema nikatoe ninapoabudu halafu pia nikatoe kwa wahitaji.

WOTE MLIOCHANGIA, NAWASHUKURU SANA.

Mm na mke wangu tulionelea tukatoe kwenye kituo cha yatima.

Si kwamba hatuheshimu madhabahu, Ni kwamba uwezo wetu kwa sasa ni duni hatuwezi kumudu kutoa sehemu zote mbili.

Hata huko kwa yatima tulikoenda tulienda kwa aibu, maana tulichonacho nikidogo mno.

Ila mkipata nafasi nendeni mkawaone hao watoto, maana kwa mujibu wa alietupokea ni kwamba several times wanalia uji.

Ni hayo tu.
ITOSHE KUSEMA AHSANTE KWA USHIRIKIANO
Mungu awabariki sana.
 
Kuna Zaka, Dhabihu na Malimbuko

Zaka - Madhabahuni kwa kuhani au Mtumishi wako anayekuhudumia...hata kama sio kanisani kwako

Dhabihu - Popote hata kwa watoto yatima, Wagonjwa, Wafungwa n.k

Malimbuko - ni Uzao wa kwanza wa mifugo yako au mazao ya kwanza katika kuvuna

Nijuavyo ni hivyo
Shida sio kujua aina za sadaka! Shida unatoa wapi? Malimbuko ni sadaka pia! Utaenda kuitoa wapi? Mimi kwasasa kutokana na mapandikizi ya mashetani yanayojiita watumishi wa Mungu, bora Katoe vituo vya wenye uhitaji kama watoto yatima na makazi ya wazee! Azarel
 
We toa popote unapotaka unachoambiwa hapa ni kuwa ili iitwe zaka ina mahali pake pa kutolewa. Ukiamua kutoa mchango wa harusi,sijui umesaidia yatima au msaada wowote ule wa kifedha we toa ila don't make a mistake of calling it ZAKA.
 
Baada ya kuomba ushauri hapa jukwaani, watu walichangia kwa hekima, kuna waliosisitiza nikatoe mahala ninapoabudu pia kuna walionishauri nikatoe kwa watu wenye uhitaji.

Pia kunawaliosema nikatoe ninapoabudu halafu pia nikatoe kwa wahitaji.

WOTE MLIOCHANGIA, NAWASHUKURU SANA.

Mm na mke wangu tulionelea tukatoe kwenye kituo cha yatima.

Si kwamba hatuheshimu madhabahu, Ni kwamba uwezo wetu kwa sasa ni duni hatuwezi kumudu kutoa sehemu zote mbili.

Hata huko kwa yatima tulikoenda tulienda kwa aibu, maana tulichonacho nikidogo mno.

Ila mkipata nafasi nendeni mkawaone hao watoto, maana kwa mujibu wa alietupokea ni kwamba several times wanalia uji.

Ni hayo tu.
ITOSHE KUSEMA AHSANTE KWA USHIRIKIANO
Hilo fungu la kumi unaweza kuligawa pia asilimia 5 kanisani 5 kwa Yakima.
Hiyo ni 10 kamili
 
Back
Top Bottom