MREJESHO: Niliomba ushauri juu ya sehemu sahihi ya kutoa fungu la kumi

Ni jambo jema ulilofanya lakini hiyo sio zaka ni sadaka nyingine tu. Zaka inatolewa madhabahuni. Lengo la zaka ni kuendeleza huduma. Kwa mantiki hiyo utapata baraka za utoaji lakini hutapata baraka za zaka kama ambavyo ziliainishwa kwenye kitabu cha Malaki. Ukitaka baraka za kutoa zaka toa zaka madhabahuni.
 
Nimejifunza kitu hapa na kimenigusa Sana mpaka chozi limetaka kunitoka , ulivyosema hakuna ndugu au majirani wenye shida, na kwa kipindi hiki Hali ngumu Sana hasa vijijini, na hata baadhi ya jirani zetu, watu wanakatiwa maji wengi mitaani ndo hapo kujiuliza Maisha yamekuwa sio Kama zamani.
 
Yani unaenda kumpa mtu hela akanunue V8 au akajenge Hotel halafu unaona umetoa sadaka wakati kuna maelfu hawana hata chakula.
Na hao ndiyo wanaharibu GDP ya nchi maana uwiano wa nguvu kazi iliyopo na kipato cha mtu mmojammoja haviwiani kutokana na wahuni wasiotoka jasho kuvuna zaidi kuliko wanaotoil mashambani
 
Mungu awabariki sana.
 
Shida sio kujua aina za sadaka! Shida unatoa wapi? Malimbuko ni sadaka pia! Utaenda kuitoa wapi? Mimi kwasasa kutokana na mapandikizi ya mashetani yanayojiita watumishi wa Mungu, bora Katoe vituo vya wenye uhitaji kama watoto yatima na makazi ya wazee! Azarel
 
We toa popote unapotaka unachoambiwa hapa ni kuwa ili iitwe zaka ina mahali pake pa kutolewa. Ukiamua kutoa mchango wa harusi,sijui umesaidia yatima au msaada wowote ule wa kifedha we toa ila don't make a mistake of calling it ZAKA.
 
Hilo fungu la kumi unaweza kuligawa pia asilimia 5 kanisani 5 kwa Yakima.
Hiyo ni 10 kamili
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…