Mrejesho: Nimesafiri na BAJA 250 XLR kupitia mbuga ya Mikumi, kwa niliyoyaona sipiti tena

Mrejesho: Nimesafiri na BAJA 250 XLR kupitia mbuga ya Mikumi, kwa niliyoyaona sipiti tena

Hahahahaaaa

Haya bana....

Inabidi tu kuzinywa hizo chai na kahawa...hata kama ni chungu

hivi we mama unajua ushaanza kuzeeka?dalili kuu ya kuanza kuzeeka ni kupenda kuchunguza kama ulichoambiwa ni kweli au lah!!!yaani wewe siku hizi kazi yako kuu ni kuchunguza thread za chai na kahawa kutwa kuchwa!!!

wenzako thread za chai tunazifurahia kichizi,thread ikinyooka inatukera tunaona bora tushinde kulekule jukwaa la siasa!dont be too serious mama life is easy
 
Hapa nipo IFAKARA nawaza naanzaje kuondoka napita wapi na BAJA Langu A.K.A ndama

Afu we jamaa muongo wa kiwango cha Nursery...! Kwenye uzi wa mwanzo kuhusu hii safari ulisema kuwa kuna viela umepata sasa umenunua gari na ukaona ni vema hiyo bodaboda uwapelekee wazee wako,sasa ukawa unaomba ushauri kama ni vema ukipita nayo mikumi.
Wengi walikushauri upakie kwenye malori particulary Fuso.

Episode II

Sehemu ya pili umeiita eti mrejesho,yaani ulikaidi ushauri wa wakuu humu ndani kwa kupita mikumi kwa kasi ya 150km/hr na bado ulifanikiwa kuona kichaka kikitisika na Simba wakatoka wakiwa na damu midomoni.

Pendekezo kwa Episode III

Kwa sasa upo ifakara umeghairi kuwapa wazee hiyo Baja hivyo umeamua kurudi nayo (labda mzee hana leseni) na unatafakari utarudi vipi. Sasa ili episode inayofuata inoge inabidi upitie njia ya kukatiza Selous game reserve unatokea ikwiriri afu huyoo tara'tiiibu unatua Dar.
Mdogomdogo mpaka Series yetu inakamilika.
 
Uongo huu unachekesha sana yaan nimecheka hadi nimepaliwa na chakula na wtt wanashangaa nacheka nn duu jf bhana ni hatari.!!!
 
Huyu hata hiyo pikipiki hana....baja 250 haina 180km/hr....ameshiba mihogo akaona aje achangamshe kijiewe.
 
Hapana hii mada ni nzuri ya kuburudisha na hadithi kama zingine
 
Mmehabarikaje Wandugu,

Nimerudi niliandika uzi kuomba uzoefu kwa waliozoea kusafiri kupitia Mbuga ya mikumi na mimi nilikuwa nataka kupita na Mwanandama wangu.

Niliondoka Moro saa 8 kwa speed ya MOTOCHINI 150 nilifika saa 9:30.Safari inaendelea nimefika Mwanzo wa mbuga naona amani tu, nimepata kujionea swala makundi kwa makundi, pundamilia na twiga kwa mbali huku tembo nao wakiendelea kutembea kwa kujigamba.

Safari inaendeleaa...., wakati bado nipo katikati ya mbuga ghafla kwenye kichaka nasikia kinatikisika ghafla simba kama watano wanatoka wakiwa wa damu mdomoni wakawa wananitizama watatu wakaunguruma huku wanafata usawa wangu nilichofanya ni kuongeza speed 180 kwani BAJA haina kujali BAMPS, wakatrot kidogo wakarudi zao, mbele kidogo mita 200 kwenye mti mkubwa namuona chui akiwa na swala kwenye mti.

Viumbe walionitisha ni Nyati waliopita kwa makundi kuvuka barabara, ilibidi nisisimame bali nirudi nilipotoka hadi nilipoona wamepita wote ndio nikapita speed 120, walirudi baadhi kunifukuzia lakini kwa kuwa wote mnamwelewa ndama alivyo.

Nilitaka kuzimia nimekutana na simba wawili mbele kulia na kushoto wawili katikati wameacha nafasi, nilichofanya ni kuwapita kama mwewe au kipanga hao nduli kwani wote mnajua mziki wao ulivyo.

USHAURI: Jamani ndugu zanguni, hapo mbugani sio pa kupita jioni wala usiku, mimi nimepita jioni mengi niliyoyaona sipiti tena, bora nipakie pikipiki kwenye lori, mnaotaka picha ni ngumu kupata labda ningekuwa nipo na wewe ukashuka kunipiga picha zingetokea vizuri.

HEBU TUAMBIE NA WEWE YALIYOKUKUTA, MIMI NILIPATA PRESSURE SIKU 3
Uongo mtakatifu na kufurahisha jamvi
1. Baja hazina spidi zaidi ya 80km/hr hata kama zimeandikwa 120km/hr
2.Kukutana na simba wawili kwa wakati mmoja, tena Mikumi ni bahati, sembuse watano,
3. Chui ndo kabisa juwezi mpata katika barabara hii halafu tena yuko mtini? Uongo mkubwa
4. Jinsi yalivyo mgari mengi mbugani yanapita barabra kuu, kumpta simba kalala barabarani mida ya jioni haiwezekani
5. Mikumi hakuna makundi ya nyati makubwa , utakuta wawili au watatu, au san sana wannne, kukuta kundi la nyati hilo halipo.

Haya mtoa mada jaribu riwaya nyingine ya kusadikika.
 
Mmehabarikaje Wandugu,

Nimerudi niliandika uzi kuomba uzoefu kwa waliozoea kusafiri kupitia Mbuga ya mikumi na mimi nilikuwa nataka kupita na Mwanandama wangu.

Niliondoka Moro saa 8 kwa speed ya MOTOCHINI 150 nilifika saa 9:30.Safari inaendelea nimefika Mwanzo wa mbuga naona amani tu, nimepata kujionea swala makundi kwa makundi, pundamilia na twiga kwa mbali huku tembo nao wakiendelea kutembea kwa kujigamba.

Safari inaendeleaa...., wakati bado nipo katikati ya mbuga ghafla kwenye kichaka nasikia kinatikisika ghafla simba kama watano wanatoka wakiwa wa damu mdomoni wakawa wananitizama watatu wakaunguruma huku wanafata usawa wangu nilichofanya ni kuongeza speed 180 kwani BAJA haina kujali BAMPS, wakatrot kidogo wakarudi zao, mbele kidogo mita 200 kwenye mti mkubwa namuona chui akiwa na swala kwenye mti.

Viumbe walionitisha ni Nyati waliopita kwa makundi kuvuka barabara, ilibidi nisisimame bali nirudi nilipotoka hadi nilipoona wamepita wote ndio nikapita speed 120, walirudi baadhi kunifukuzia lakini kwa kuwa wote mnamwelewa ndama alivyo.

Nilitaka kuzimia nimekutana na simba wawili mbele kulia na kushoto wawili katikati wameacha nafasi, nilichofanya ni kuwapita kama mwewe au kipanga hao nduli kwani wote mnajua mziki wao ulivyo.

USHAURI: Jamani ndugu zanguni, hapo mbugani sio pa kupita jioni wala usiku, mimi nimepita jioni mengi niliyoyaona sipiti tena, bora nipakie pikipiki kwenye lori, mnaotaka picha ni ngumu kupata labda ningekuwa nipo na wewe ukashuka kunipiga picha zingetokea vizuri.

HEBU TUAMBIE NA WEWE YALIYOKUKUTA, MIMI NILIPATA PRESSURE SIKU 3
Nimepita Mikumi zaidi ya mara moja kwakweli siogopi kupita tena na tena. However huwa napita wakati wa jua kali.

Wakati mmoja wakati napita nilihofia tu kugonga viumbe wa watu maana faini zimeandikwa, ila sio kuogopa kuliwa kisa nipo kwenye pikipiki.

Na napanga kupita tena mwaka huu
 
Back
Top Bottom