Mrejesho no 2: Mtoto wa kiume umri miaka 10 anakojoa mkojo umechanganyikana na damu

Akachunguzwe figo zake kama sipo salama


Huenda pia alikuwa na UTI ya muda mrefu na hakupata matibabu sahihi hivyo ikapelekea infection ifike mpaka kwenye figo (Pyleronephritis) , au huenda pia amepata nephritic syndrome.

Je mtoto huwa uso unavimba haswa nyakati za asubuhi?

Na mkojo vipi anapata mwingi au umepungua na wenyewe ?
 
Je mwanao miguu yake inavimba au uso wake unavimba?, na hapo nyuma alishasumbuliwa na ugonjwa wa kukohoa au maambukizi ya Njia ya hewa.
Mambo ya post streptococcus glomerular nephritis.

πŸ”₯πŸ”₯πŸ”₯πŸ”₯
 
Tangu kaanza kukojoa damu mkojo umepungua
 
Nawasiwasi kweli kuwa figo haziko salama,haijawahi kuugua UTI ila nahisi atakua labda ana UTI mda mrefu na hatujui
Kuhusu kuvimba mtoto havimbi asubuh ila ana uso wenye mashavu makubwa
Kabla yakuanza kuugua hiyo jumatano,mkojo alikua anapata mwingi tu ila baada kuanza dawa alhamis mkojo umepungua na imekua unatoka wadamu tu
 
Tukapewa dawa ya kichocho plazquantel 600mg yaan vidongo 4 vya mg600,
Vidonge 4, Ana umri/uzito gani huyo mtoto?? πŸ€” πŸ€”

dawa hii ya NITROFURANTOIN-100mg atakunywa 1Γ—2,
Hii dawa mgonjwa anapewa kulingana na uzito,. Naona kuna mis-diagnosis.


Au ulienda hospital za hapa na pale, πŸ˜’πŸ˜’
 
Niko mkoa wa tabora,nawaza kwenda hospital kati ya dar au dom Sasa niende hospital ipi ndo nasubiria mawazo yeny
Uko tabora si uende bugando? Maana ndio hospitali kubwa ya ukanda huo kuliko kwenda mbali zaidi na hospitali kubwa iko hapo!
 
Vidonge 4, Ana umri/uzito gani huyo mtoto?? πŸ€” πŸ€”


Hii dawa mgonjwa anapewa kulingana na uzito,. Naona kuna mis-diagnosis.


Au ulienda hospital za hapa na pale, πŸ˜’πŸ˜’
Kaenda hospital ya rufaa hospital ya mkoa ana umri wa miaka10
 
Oooh...ni "praznquantel"?Songwe kutokucheza kwenye maji machafu(?)ya vidimbwi,mito,mitaro na yoyote yaliyo hatari kwa afya.
 
Niliwahi kupata hilo tatizo, mara mbili, wakati ninaishi Mvuha. Iko hivi, hapo mtoto wako slipo anapata maumivu makali sana chini ya kitovu, chapati choo kizuri, moja moja kwa moja twende kwenye tatizo, mpaka hapo mwanao anaumwa kichocho kikali, na hiyo damu uoonayo ni kwamba bacteria maambukixi yamefika kwenye kibofu cha mkojo, hizo ni chembe za damu ndio zinaleta huo wekundu. Nakumbuka nilichomwa sindano na nikapewa dawa za kumeza, Ndugu baada ya kutumia dawa zilipita siku kama tatu ndio nilianza kupata dalili za kupona, nakumbuka Tiba ilichukua wiki nzima. Hapo mtoto anapata maumivu makali sana kwenye kibofu. Inatibika, kwa Morogoro mjini mimi nilipata matibabu hospital mbili tofauti, mara ya kwanza nilizani ni kichocho cha kawaida nilienda zahanati binafsi nikaandikiwa dawa na sindano nikapona, lakini baada ya kukaa muda fulani tatizo lilirudi, nikaenda pale platinum iko msamvu ndipo hapo nikaambiwa kibofu cha mkojo kina infection. So ni kichocho ambacho kimefika kwenye kibofu Kaka. Atapona ila mpambanie dogo anapata maumivu makali mnoo.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…