Mrejesho no 2: Mtoto wa kiume umri miaka 10 anakojoa mkojo umechanganyikana na damu

Mrejesho no 2: Mtoto wa kiume umri miaka 10 anakojoa mkojo umechanganyikana na damu

Kwaiyo hapa nini kifanyike mkuu
Mkuu mimi huwa sipendi sana kutoa diagnosis kwa njia ya kupiga ramli,

Jambo la msingi ni kupata majibu yaliyo sahihi ili tiba iendane na ugonjwa.

Kama majibu hayaeleweki, Nenda hata shinyanga pale hospital ya mwawaza, au kambarage Hospital ipo shinyanga mjini karibu na stend, au nenda mwanza kamanga ipo pale nyegezi, au bugando
 
Habar wakuu,kama nilivyoleta kwenu ugongwa huo wa mtoto wangu nanikachukua hatua yakwenda hospital ya rufaa akapimwa mrejesho wa kwa kwanza kipimo katika mkojo usio na damu hakuonekana nitatizo,vipimo vya siku ya pili akapimwa mkojo uliokuwa umechanganyikana na damu majibu yakatoka ana kichocho
Tukapewa dawa ya kichocho plazquantel 600mg yaan vidongo 4 vya mg600,mtoto akaanza kutumia usiku wa juzi,usiku huo huo alikojoa mkojo kiasi Cha kikombe Cha kahawa baadae asubuh ya Jana akanywa kidonge Cha pili,
Sasa kuanzia hapo asubuh ya Jana mpaka jioni akawa amekunyw amekunywa maji kiasi Cha Lita moja na nusu lakini wakati wote mkojo anakojoa wenye damu kabisa,Sasa Leo asubuh amemalizia kidogo Cha mwisho,nakuazia asubuh hiyo Hadi kufikia usiku huu amekunywa maji jumla Lita1.5 lakini mkojo Amekua anakojoa kidogo kidogo katika makopo mkojo wenye mchanganyiko na damu Sasa nimeukusanya mkojo wote waleo siku mzima ambappo amekunywa maji Lita moja na nusu
Na asubuh ya kesho ataanza dawa hii ya NITROFURANTOIN-100mg atakunywa 1×2, Leo asubuh dawa ya prazquantel 600mg amemalizia ila Hadi Sasa anakojoa damu naambatanisha nipicha ya mkojo ameokojoa siku mzima baada ya kunywa maji lita1.5
Msaada wenu nimpeleke hospital Gani kubwa Zaid ambayo inawataalamu watakao baini nakulimaliza tatizo la mtoto wangu
Pia hospital hizo kubwa nikaonane na daktar anaetibu magonjwa yepi
Gentleman,
nashauri,
baada ya dozi kwisha,
ni muhimu kuvuta subra walau kwa wiki moja zaidi, huku kijana akiendelea kula na kushiba vizuri huku akiendelea kunywa maji ya kutosha na matunda yenye maji kwa wingi.

dozi aliyotumia ni very strong,
ni vizuri pakawa na interval kidogo kabla ya kuanzishwa dozi nyingine ili kuepuka kuzalisha changamoto nyingine mpya inayoweza kutokea kutokana na athari za madawa mengi mfululizo.

Aidha,
ni vizuri kumchunguza Figo, huenda damu inayoonekana kwenye mkojo inatoka kwenye figo inayovuja kutokana na sababu mbalimbali.
Hata hivyo ni muhimu zaidi kuzingatia ushauri wa daktari mahalia.

Gentleman,
Mwenyezi Mungu akufanyie wepesi, na amjalie nafuu na hatimae uponyaji wa mapema kijana wetu.🌹
 
Mpeleke hospital ya serikali ngazi ya wilaya mkoa au kanda ,

Lakn mtoto mnampa maji mengi mno 1.5L per day anatak mwenyew ? (Kama ni yeye mwenyew anatak ni saw
 
Mpeleke hospital ya serikali ngazi ya wilaya mkoa au kanda ,

Lakn mtoto mnampa maji mengi mno 1.5L per day anatak mwenyew ? (Kama ni yeye mwenyew anatak ni saw
Mtoto imebainika sio kichocho
 
Mrejesho majibu ni haya ya ultrasound yamebaini ugonjwa ila hana kichocho
 

Attachments

  • IMG_20260921_141711.jpg
    IMG_20260921_141711.jpg
    338.3 KB · Views: 13
Mrejesho majibu ni haya ya ultrasound yamebaini ugonjwa ila hana kichocho
Kuna dalili za maambuzi ya bacteria kwenye figo(pyelonephritis) yametoka kwenye kibofu hadi kwenye figo
 
Akachunguzwe figo zake kama sipo salama


Huenda pia alikuwa na UTI ya muda mrefu na hakupata matibabu sahihi hivyo ikapelekea infection ifike mpaka kwenye figo (Pyleronephritis) , au huenda pia amepata nephritic syndrome.

Je mtoto huwa uso unavimba haswa nyakati za asubuhi?

Na mkojo vipi anapata mwingi au umepungua na wenyewe ?
Mkuu majibu ya ultrasound haya hapa
Kuna dalili za maambuzi ya bacteria kwenye figo(pyelonephritis) yametoka kwenye kibofu hadi kwenye figo
Hapa nin chakufanya
 

Attachments

  • IMG_20260921_141712.jpg
    IMG_20260921_141712.jpg
    381.9 KB · Views: 12
Kuna dalili za maambuzi ya bacteria kwenye figo(pyelonephritis) yametoka kwenye kibofu hadi kwenye figo
Hapa niende hospital Gani kwa dar ntakayopatiwa tiba sahihi akapona mtoto
 
Hapa niende hospital Gani kwa dar ntakayopatiwa tiba sahihi akapona mtoto
Sina uzoefu nenda MUHIMBILI , KAILUKI ,
Hao waliompima mtoto hawajakwambia uende hospital gani kama kwao hawezi ku dili na hilo Tatizo, na wew c upo jiji (dar
 
Nenda Kairuki, Muhimbili nk ila ushauri wangu unabaki palepale, fanya matibabu ya kimwili, pia mtoto apate maombi.

Kuna mambo mengi sana duniani.
 
Sina uzoefu nenda MUHIMBILI , KAILUKI ,
Hao waliompima mtoto hawajakwambia uende hospital gani kama kwao hawezi ku dili na hilo Tatizo, na wew c upo jiji (dar
Muhimbili ipi mloganzila au upanga
 
Back
Top Bottom