Mrejesho no 2: Mtoto wa kiume umri miaka 10 anakojoa mkojo umechanganyikana na damu

Mhhhh, kazi kweli kweli, hii management imenishangaza sana, kwa hospital kubwa kama ile.. Usije ukawa ulienda "amen",
Mkuu nimeenda kitete na siku mbili mfululizo siku yakwanza wakasema hakuna ugonjwa,siku ya pili nikarud na sample ya mkojo wakapima tena
 
Ulikuwa na umri gani?
Mtu mzima ngumu kupata kichocho sababu aogelei kwenye madimbwi na mabwawa, maji yasiyotembea.
 
Mkuu nimeenda kitete na siku mbili mfululizo siku yakwanza wakasema hakuna ugonjwa,siku ya pili nikarud na sample ya mkojo wakapima tena
Basi wameetibu kwa uzoefu baada ya kuona tatizo halionekani.. 🀝 🀝
 
Wallah!?Vema sana.Tukutuku au uwanja wa dhambi unapafahamu?
Tukutuku, machinjioni, kizigo, ng'ambo, Livingston unaoelekea kwihala, kigamboni, tabora boys na girls, kaze-hill, TBC, CG FM, cheo A na cheo B, ipuli kule mitaa ya freemason, chemchem, unapnda kule juu jeshini, kwa mrema kwenye kitimoto kule. πŸ˜…πŸ˜…πŸ˜…πŸ˜…
 
Ulikuwa na umri gani?
Mtu mzima ngumu kupata kichocho sababu aogelei kwenye madimbwi na mabwawa, maji yasiyotembea.
Huwa Siogelei kwenye mito wala madimbwi.

Hapo nilipokuwa naishi kwa wakati huo, maji yalikuwa ni ni issue, sijui kwa sasa, hivyo kuna watu wanachota maji mtoni na kuja kuyauza mtaani, baada ya kuumwa mara ya kwanza nikapona kabisa ila sikuambiwa tatizo ni nini, lakini awamu ya pili ilipojirudia nilienda sasa Hospital inayoeleweka nikafanya vipimo vyote ndipo wakagundua shida iko kwenye kibofu.

Kule mtoni kuna mambo mengi, wapo wanaosafishia dhahabu humo, wapo wanaokojoa humo, wapo wanaofua humo, wapo wanaoshusha haja kubwa humo.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…