Mr Dudumizi
JF-Expert Member
- Sep 9, 2020
- 7,799
- 14,215
Habari zenu wanaJF wenzangu,
ONE 1:
Kwanza naomba nitumie nafasi hii kumshukuru kiongozi mkuu wa mtandao wetu huu Mhe. Maxence Melo na team yake nzima ya JF kwa kuuboresha mtandao wetu, hadi kufikia level ya kimataifa. Mtandao huu umekuwa sauti kwa watu wasiokuwa na sauti, umekuwa mtetezi kwa watu wasiokuwa na watetezi, na umekuwa msaada kwa watu waliofeli kusaidiwa.
Hakika kama una ndugu yako, rafiki yako au mtu ambae una ukaribu nae ila sio member wa JF, basi tumia undugu, urafiki na ukaribu wako kwake kumshauri ajiunge JF, hakika hatojutia na kuna siku atakuja kukushukuru mno kwa hilo.
TWO 2.
Pili nauomba uongozi wa JF wasiuunganishe uzi huu na ule wa mwanzo ambao nimeuleta siku kadhaa za tukio la kwanza lilipotokea. Ni bora waweke kichwa cha habari cha uzi hapo chini, ili kama kuna mtu ambae hakuwahi kuusoma ule wa mwanzo, basi aupitie na kurudi kuendelea na huu wa leo.
Pia nawashukuru members wote wa JF waliochangia kwa namna moja au nyingine kile walichoona ni bora katika kumsaidia mtoto yule aliekuwa anateseka bila hatia yoyote, kwa wazazi wake (mmoja) wa kumzaa, (mungine) wa kambo.
MREJESHO:
Jana jioni mida ya saa 12:30 nikiwa nimetoka zangu mahangaikoni, baada ya kuoga na kujipumzisha sitting room huku nafuatilia vipindi mbali mbali vya TV, sim yangu ina ring. Nanyanya kuangalia naona ni namba ya yule home boy (baba mtoto). Kwanza nikaacha kupokea nikijua hakuna lolote la maana atalonambia zaidi ya kile kile cha kunishtumu kumuhonga mkewe nguo, so nikapotezea. Baadae ikakata kisha nikaona ametuma meseji ikisema tafadhali kaka naomba pokea tuongee mara moja.
Hiyo meseji ikanifanya nipate moyo wa kuchukua sim yangu na kumpigia. Alipoitika baada ya salam, nikamuuliza kuna nini tena la zaidi ambalo limemfanya anipigie sim, wakati alikuwa ameshanionya kwamba mimi na yeye urafiki wetu umefika mwisho, tusijuane na wala tusitembeleane.
Jamaa akashusha pumzi na kuniomba nimruhusu aje nyumbani tuzungumze. Moyo ulitaka kusita, lkn nikafikiria ukaribu wetu tuliokuwa nae mimi na yeye, pia nikaona huenda ukaribu wetu ukarudia na kuitumia njia hiyo kutafuta namna ya kumsaidia mtoto wake zaidi, kwani yeye ni kama vile haoneshi kuwa na msaada wowote kwa mtoto wake kama mzazi. So nikamjibu poa tu unaweza ukaja. Akauliza hata sasa hivi? nikamjibu ndio, akasema poa, na mimi nikakata simu.
Sikumwambia shemej yenu chochote, maana kuna mambo ambayo ukikimbilia kumshirikisha mke unaharibu kila kitu. Japo wakati tunaongea na home boy yeye alikuja karibu, na kutaka kujua naongea na nani, na tunaongelea nini, nilimfukuza nikamwambia aende jikoni akaniandalie chakula haraka ili niwahi kula na kupumzika. Aliondoka pale shingo upande ila ndo hivyo mume nimeshaongea, hana namna ya kupinga wala kukataa.
Baada ya dakika kama 30 hivi mwamba akanipigia tena kuwa yupo nje. Nikamwambia nakuja, kweli nikamkuta nje akiwa na his son. Nikawakaribisha ndani. Wife kuwaona uso ukabadilika ila hakutaka kuonesha hilo mbele ya shemej yake (lakini mimi) nikawa nimeshabaini kila kitu.
Basi wakaingia ndani, mtoto kuwaona wenzie mbio akawakimbilia wakakumbatiana na kufurahiana pamoja. Sisi kwanza tukabaki kuwaangalia na kutazamana. Ni kama vile rafiki yangu aliguswa na lile tukio, uso wake ukawa mfano wa mtu alieletewa habari ya msiba. Wife akamletea juisi anayopenda kunywa, na mimi akaniletea Glass ya maziwa tukawa tunakunywa, kila mmoja akimuuliza mwenzake habari za kazi na kutwa nzima ya siku ile nk.
Baada ya mazungumzo yetu ya kawaida ya hapa na pale. Ndo jamaa akaanza kuniambia kuwa sasa amefahamu ukweli wa mateso anayopitia mtoto wake kupitia ndugu zake waliopo bongo, pamoja na mtoto mwenyewe. Nikamuuliza amejua ukweli kupitia ndugu zake waliopo bongo kivipi na namna gani aliupata ukweli huo?
Akanambia kwamba kuna ndugu zake ambao ni members wa jukwaa hili la JF. Waliposoma thread yangu na kuonganisha dot ya kodi nilizoweka kama vile kufiwa na mke, kuachiwa mtoto wa miaka 4 na sasa ana miaka 7, kuowa mkongo na sehem alipozaliwa Bongo, kuliwafanya waunganishe dot na kumpigia sim kumuuliza ndugu yao kama kuna jamaa mtz aliwahi kugombana nae siku mbili hizi, pamoja na swala la kudaiwa na mkewe kudai kununuliwa nguo na mtz huyo nk. Home boy akawajibu ndio, ila na yeye akashangaa jinsi walivyozipata taarifa hizo na wakati ndugu hao mimi binafsi nilikuwa siwafahamu.
Ndio ndugu hao wakamwambia kuwa habari hizi walizipata kupitia katika mtandao wa JF. Na kuamua kumtafuta na kumuuliza kama hili swala linahusiana na yeye au ni mtu mungine. Kwa bahati nzuri wakakuta ni yeye. Huu mtandao jamaa niliwahi kumshauri ajiunge ili apate taarifa ya mambo mbali mbali yanayotokea duniani, Na pia ajifunze mambo ambayo hayafahamu, ila kwa bahati mbaya aliniambia kwamba yeye hayupo interested na mambo ya mitandao, so nikamuacha.
Baada ya kupewa maelezo na ndugu zake kuhusu kila kitu kilichoandikwa, ikabidi atafute sehemu sahihi na kumuuliza mtoto wake kinachomsibu pale nyumbani na kumuahidi mtoto wake huyo kumpa zawadi ikiwa atamwambia ukweli wa kile anachofanyiwa na mama yake wa kambo. Mtoto ashaahidiwa zawadi tena na baba mzazi. Akamwaga kila kitu, jamaa anadai hadi alijikuta machozi yakimtoka na kumkumbuka marehemu mkewe ambae alimsihi mume wake huyo kuhakikisha anampenda mtoto wao huyo pindi atapochukuliwa na alietuleta hapa duniani (Mungu), hapo mkewe alikuwa hospital na uwezekano wa kupona ulikuwa ni 0%. Jamaa akakubali na kumuahidi mkewe kuwa atakuwa tayari kumpenda Na kumpigania mtoto wao huyo hata kama kumpigania huko kutachukua maisha yake potelea mbali as long as mtoto atakuwa salama salmin.
Home boy akasema kilichomleta kwanza ni kuomba msamaha kwangu na familia yangu. Pili ku confirm kutoka kwangu na mtoto. Nikamtuliza nikamwambia kuwa siku zote mzazi iwe baba au mama unatakiwa kabla ya kulala hakikisha unapata muda kidogo wa kuongea na watoto wako ili ujue kinachowasibu kwa siku nzima ambayo wewe haukuwa karibu yao. Kwa kufanya hivyo utakuwa unajiweka karibu na watoto kisha utafahamu mambo mengi ambayo wanayafanya au kufanyiwa watu mbali mbali majumbani, mitaani au shuleni.
Baada ya maongezi yale na kusameheana jamaa akaaga,, ila akaomba nikae na mwanae ili acheze na wenzake, yeye angekuja kumchukua asubuhi. Nikaona hilo halina shida maana hata wenzake walikuwa wamesha mmisi. Basi mwamba akaondoka.
Haikupita hata masaa mawili naona shemej (mkewe) ananipigia sim. Nilitaka kuacha kuipokea ila wife akaniomba niipokee ili nimsikilize atachosema. Ile kupokea nasikia mtu analia kwamba niende nikamsaidie, eti rafiki yangu anataka kumuua ashampiga mpaka kamtoa meno mawili nk. Nikaona bora na yeye leo apigwe na kusikia uchungu wa kupigwa kama alivyokuwa anasikia uchungu mtoto wa kambo. Nikamjibu kuwa nipo mbali kidogo na nyumbani, hivyo siwezi kuwa msaada kwake. Akiwa bado analalamika nikasikia simu imekata ghafla, kumbe home boy alimpora sim Na kuivunja. Tukawa tunafurahi na mke wangu. Ghafla mlango wetu ukawa unagongwa, nikauliza nani, kumbe shemej mke wa jamaa.
Wife akawahi kufungua na kukuta damu zikimtoka mdomoni, mapuani, kichwani na sehemu mbali mbali za mwili. Wife akamuuliza kilichomleta eti anaomba hifadhi ya usiku mmoja. Wife akwambia kwangu hakuna hifadhi kwa mtu mwenye roho ya shetani na kumtaka aondoke kabla na yeye wife hajamuanzishia kipigo. Nilijikuta nacheka mwenyewe ndani baada ya kusikia na wife nae anataka kumuongezea kipigo (wife ana hasira za karibu) na akiamua jambo hatanii. Mkongo akaona bora atoke akaombe hifadhi sehemu nyingine tusioifahamu.
Asubuhi mwamba kaja na yule mtoto wake mungine mdogo aliezaa na mama wa kambo ambae alikimbia kipigo na kumuacha. Nikamwambia wife amtizamie mara moja akitoka kazini usiku atakuja nyumbani kumchukua.
Mama shemej wa Congo sijui alilala wapi, na haijulikani kwa sasa yuko wapi. Yote nitayafahamu vizuri nitapofika nyumbani kutoka kazini. Japo sikupenda kumuachanisha rafiki yangu na mkewe, lakini hatua aliyochukua ni ya kiume na kiutu. Nimempongeza sana aisee.
Mada ya Mwanzo: Rafiki yangu kanipa kesi, kisa nimemsaidia mtoto wake mwenyewe