Mrejesho wa thread ya rafiki yangu alienipa kesi, kisa nimemsaidia mtoto wake. Jana kafanya jambo ambalo mkewe hatokuja kulisahau maishani kwake

Wewe pia ni mpumbavu. Mtu kupigwa na kutolewa meno mawili unaona ni sawa? Una tofauti gani na hawa watekaji wanaoumiza watu?
Mkuu huu ni uzi wa pili. Ukirudi kule kwenye thread kwa chini kabisa utaona kuna uzi wa kwanza ambao huyo mama alisababisha mateso makubwa kwa mtoto yatima wa miaka 7. Kila binadam ana haki ya kuishi kwa amani na furaha.

Haiwezekane yeye amtese mtoto wa mwenzake kwa kipigo, kumnyima chakula na mateso mengine kibao. Halafu baba mtoto agundue na kurudisha kichapo eti mimi nimuonee huruma. Hapana mkuu. Hilo bila unafiki nalikataa. Ukiona mtu anakushangaa kwa kumpiga mwizi, ujue hajawahi kuibiwa huyo.

Hivyo wewe sikushangai kwa kumtetea huyo mama, ni kwa sababu machungu na mateso aliyopata huyo mtoto wewe huyajui.
 
Hongera kwa kazi nzuri...uzi wako mara ya kwanza nilipousoma,ulinitia majonzi sana...kiukweli huyo mwanamke,ni zaidi ya Mzee shetani.Alivyopigwa,safi kabisa....Mavi yake...
 
Mkuu,aliyeandika hapa kukuita wewe mpumbavu,ni yule mama wa kikongo...mtesaji wa mtoto.Achana nae.Bwege mtozeni ...muache tu.Na bado....ngoja wakung'oe jicho urudi kongo chongo...🤣
 
Kama chai chai hivi!
Lakini poa tunainywa hivyo hivyo, hongera lakini kwa moyo wa upendo na kujali.
Sio km ni chai, hapo alipoanza kusema sijui JF imefanyaje na kushauri ajiunge blah blah nyingi za ndugu kumsoma jeiefu nikaona mufindi hii hapa 🤣🤣🤣
 
Hongera kwa kazi nzuri...uzi wako mara ya kwanza nilipousoma,ulinitia majonzi sana...kiukweli huyo mwanamke,ni zaidi ya Mzee shetani.Alivyopigwa,safi kabisa....Mavi yake...
Shukran mkuu, halafu eti kuna watu wananilaumu kwa kushangilia huyu mwanamke kupigwa na kuacha kumsaidia. Hivi mwanamke shetan wa namna hii ni wa kusaidia kweli!!
 
Isingewezekana kumtwanga mke wa mtu hivi hivi. Ata kipigo alichopata kutoka kwa mumewe kinatosha kumfunza namna ya kuishi na mtoto wa kambo 🤣🤣🤣
Huyo hatakiwi kurudishwa na rafiki yako. Bora atafute mke mungine.
 
Unajisikiaje kuandika paragraphs tatu kutetea upumbavu? Uzi wako wa kwanza haukuwa na shida. Shida inaanza kwa wewe kuona sawa mtu kung'olewa meno na kujeruhiwa vibaya. Una tofauti gani na waliomuua Mzee wa CHADEMA? Yaani wewe na huyo jirani yako ni wapumbavu sana mnaoweza kujikuta jela kizembe kwa kukosa akili. Huyo mama akienda mahakamani huyo jirani yako atakuwa na kesi ya jinai ya kujibu.
 
Ok ila jamaa ndo ashaenda polisi na mtoto kumfungulia huyo mama kesi ya kumtesa, kumnyima chakula na kumpiga huyo mtoto kila siku.

Mtoto kahojiwa na kuonesha alama mbali mbali zilizosababishwa na kipigo, pamoja na adhabu kutoka kwa huyo mama yake wa kambo. Jamaa kapewa RB na huyo mama anatafutwa. Wakishafika mahamani ndo tutajua nani ana haki kati ya mtoto, mama wa kambo au baba mwenye nyumba.
 
Wewe ni jembe kudadeki,Tena umefanya kitu kikubwa sanaaaa.Bora waachane na huyo mmama atadanga na atapata kuendesha maisha yake kuliko kumtesa mtoto mdogo asiyejua kesho yake wala wapi pa kwenda Zaid ya kumuharibu kisaikolojia TU.

Hyo ndo dawa
 
Kama huyo mama hajaripoti polisi atakuwa ni mpuuzi asiyejua haki zake. Wewe pia uko vizuri kwenye tasnia ya umbeya. Badala ya kupatanisha watu unafurahia familia kubomoka. Ungekuwa ndugu yangu ningekutenga.
 
Umevunja ndoa ya watu
Mi niliamua ku mind my own business majirani hata wakiuwana mi ndio navuta shuks
Hiyo ni kweli ila wakati mwingine ni vizuri kujuwa kinachoendelea labda uwepo wako unaweza kuokoa maisha ya mtu.
 
Tatepa Baba.
Mtaalam wa kusuka hisia kwa maneno Mr.Dudumiz all the way from Migo Migo.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…