High Vampire
JF-Expert Member
- Nov 17, 2012
- 2,915
- 2,134
Nataka lipa ya tigo Pesa inawezekana kupata?
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
UKIWA NA TIGO UNAWEZA USIZIME DATA KWA HIZI BANDO ZENYE UNAFUU MNOO‼️Nataka lipa ya tigo Pesa inawezekana kupata?
Nikuulize inakuwa unlimited kweli bila kupunguza kasi, au kuishia njiani kutokana na matumizi yako kwa maana niliona hawa Voda wanaujanja,unpodownload spidi hupunguza ukilinganisha na kuupload na sisi huku tunadownload zaidi kuliko kuuploadWakati kwa 115,000 unapata unlimited ya voda
Mkuu nashukuru sana kwa kunionesha hili chimbo maana hawa wezi Halotel wananiumiza kichwa!Nipo natumia huduma hii tangu mwaka jana na msukumo wa kuja huku ilikuwa ni baada ya mitandao kupandisha bei za mabando, nadhani wote mnakumbuka mabando yalikuwa bei chee ila kuna wabongo hawakutosheka wakaanza kuyabipu makampuni ya simu kwamba vifurushi visiwe vina expire, Mb ni chache, n.k. ishu ikafika hadi wizarani ikawa ajenda kubwa, mitandao ikapiga na ndio ukawa mwanzo wa vifurushi kuuzwa bei kali, hakika huwezi jua thamani ya ulichonacho hadi kipotee!!
Ok back to the topic, Nipo na hawa tigo since last year na huu ndio mrejesho wangu.
Kupunguza gharama za internet - Kila mwez naungwa GB 80 kwa shilingi elf 60, hii ni sawa na shilingi 750 kwa kila GB, kwangu ni deal safi kabisa sijui kabisa mambo ya kuzima data,
kumekuwa na mabadiliko ya bei kwa wateja wapya lakini sisi wateja wa zamani hatuguswi na mabadiliko, kwa sasa wateja wapya bei zao hizi hapa.
View attachment 2642869
Upigaji / Wizi - Kuna ule upigaji unakuta umejiunga gb 1 ila ukitumia MB 300 tu unaambiwa bando limeisha au unatumiwa sms kwamba umetumia 75%, Huku sijaona hicho kitu, Natumia router inayohesabu nimetumia gb ngapi, na nikiangalia salio kwenye mtandao kweli naona kuna uwiano. Mfano kwa hapa Kwenye router umetumija GB 2 na MB 207, kwenye salio la tigo inaonyesha zimebaki GB 77 na MB 793, kwa kifurushi changu cha GB 80 pana uwiano.
View attachment 2642874
View attachment 2642890
Speed - Mwanzoni speed nilikuwa napata changamoto nikitumia internet nyumbani nje kidogo ya mji tofauti na nikiwa ofisni sehemu za centre, yani nikifika home nlikuwa napata speed ndogo sana tena ikifika usiku ndio naweza kuzima kabisa, kipindi hiki nilikuwa natumia line yao kwenye simu yangu ya Samsung iliyokuwa na laini 2, Ndipo nilipokutana na kijana wetu wa IT ninapofanyia kazi akanishauri ninunue pocket router sababu ni kifaa maalum kwajili ya kukusanya mawimbi ya Net, Hio router ni 75,000 lakini niliingia group la facebook la mkoa nilipo nikapata iliyotumika kwa 20,000, niliongezea elf 10 ya mwanasheria kutuandalia mkataba wa kuuziana (mkataba unilinde endapo router ni ya wizi).
niliambiwa niiweke dirishani ila kwa eneo nilipo speed ilipanda kidogo, kijana wa IT alikuja nyumbani kwangu akakonnect wifi anadownload muvi kwenye simu yake huku anatembea na router anaipitisha maeneo kadhaa ya mle ndani anacheki sehem yenye speed kubwa, alipoiweka juu ya mlango speed ikafika MB 2 kwa sekunde, ndio sehemu nayotegesha router kila niwapo nyumbani.
View attachment 2642928
Malipo - Kila Tarehe 1 inapofika bando linaingia , Napewa siku 9 za kukamilisha malipo kuanzia tarehe 1 hadi tarehe 9.
View attachment 2642865
Mobility - Niliwahi fikiria kufunga nyumbani fibre ya ttcl elf 50 kwa mwezi unlimited, tatizo likawa ni mobility (utumiaji wa sehemu zaidi ya moja) ndipo paliponishinda, pia umeme ukikatika haitumiki, nguzo zikidondoka hakuna huduma, n.k. ni tofauti na post paid nabeba ki router changu sehemu yoyote napoenda hata nikiwa na drive.