Mrembo albino ajiondoa katika mashindano ya Miss Mwanza

Mrembo albino ajiondoa katika mashindano ya Miss Mwanza

Pdidy

JF-Expert Member
Joined
Nov 22, 2007
Posts
57,951
Reaction score
32,619
Mrembo albino ajiondoa katika mashindano ya Miss Mwanza

Na Paulina David, Mwanza

MREMBO Grace Wabani (23) amejiondoa kwenye mashindano ya kumsaka mrembo wa Mkoa wa Mwanza yanayotarajia kufanyika Juni 5 mwaka huu katika Uwanja wa CCM, Kirumba jijini hapa.

Grace ambaye ni mlemavu wa ngozi (albino) amejiondoa katika mashindano hayo kutokana na kile alichokieleza kuwa amejikuta akitumia muda mwingi katika maandalizi ya mashindano hayo na hivyo kukosa muda wa masomo.

Alisema kutokana na hali hiyo ameogopa kurudia mwaka kutokana na kushindwa kufanya vizuri katika mitihani yake.

Mie sikujua kama mashindano ya U-Miss mtu anatumia muda mwingi sana katika maandalizi, lakini nilipogundua kuwa muda mwingi unatumika na masomo nimesimama nimeona niache tu kushiriki ili niendelee na masomo,î alisema

ìUnaju mie nilikuwa sijafanya baadhi ya mazoezi na hivi sasa tunajiandaa kwa ajili ya mitihani ya mwisho wa mwaka sasa kama nitashindwa kufanya vizuri kwenye mitihani yangu ni wazi kuwa nitarudia mwaka, jambo ambalo litanipotezea muda,î alisema Grace

Alisema kuwa yeye ni mwanafunzi wa mwaka wa kwanza katika Chuo Kikuu cha Mtakatifu Augustine (SAUT), akisomea masomo ya ugavi na kwamba kuacha kwake kushiriki mashindano ya urembo hakuhusiani na shinikizo la mtu yoyote, bali ni maamuzi yake binafsi baada ya kupima uzito wa masomo na urembo.

ìMie najua watu watasema mengi , lakini ukweli nimeangalia faida ya kushiriki mashindano ya urembo halafu nirudie mwaka ama kuacha kushiriki halafu niendelee na masomo, nikaamua kuchagua,î alisema.

Kwa upande wa mratibu wa mashindano hayo, Flora Lauwo amethibitisha mrembo huyo kujiondoa kwenye mashindano hayo ya urembo tangu Mei 31 mwaka huu.
 
Alikuwa anatafuta upedezheee huyo.
Lakini bora amethubutunampa kudos
 
ajiondoa au kambiwa ajiondoe na chuo chake ?

mbona mnataka kuchanganya watu?

shule yake imemwambia ajiondoe
 
Yaani hiki chuo wako low sana!

Ni chuo cha dini nini??

Wako low sana lakini si ndio hao darasa zima liliitwa kwenye usaili kuhusu kazi moja hapo kwenye bunge tukufu la jamhuri muungano inayotishiwa na kuparaganyika ya Tanzania?
 
Jamani angeshinda? ama ndo alikuwa anataka jipandisha chat?
 
Jamani angeshinda? ama ndo alikuwa anataka jipandisha chat?

Hard to tell. Ongea na Lundenga akupe vigezo vya washiriki. Lakini naamini kama alikuwa amekubaliwa kushiriki mpaka mazoezi basi ana vigezo vyote. Basi angeweza kushinda na kupanda chart. Lol!
 
Grace jana alishiriki mashindano hayo na kufikia hatua ya kumi bora. Jambo lililojitokeza ni kuwa alikuwa anashangiliwa sana alipokuwa anapanda jukwaani.
 
Poa sana yani: hata mimi ningemshangilia huyo mrembo!!
Ni kweli kabisa. Ilikuwa kama message kwa wale washirikina kuwa walemavu wa ngozi ni ndugu zetu na tunawapenda sana kama tunavyojipenda sisi na wanayofanyiwa yanatukera sana.
 
Grace jana alishiriki mashindano hayo na kufikia hatua ya kumi bora. Jambo lililojitokeza ni kuwa alikuwa anashangiliwa sana alipokuwa anapanda jukwaani.

Sasa mbona stori ipo miguu juu kichwa chini wajameni? au macho yangu?
 
Grace jana alishiriki mashindano hayo na kufikia hatua ya kumi bora. Jambo lililojitokeza ni kuwa alikuwa anashangiliwa sana alipokuwa anapanda jukwaani.

Sii wanasema amekatazwa kushiriki?

Ukweli ni upi?
 
Chakaza said:
Grace jana alishiriki mashindano hayo na kufikia hatua ya kumi bora. Jambo lililojitokeza ni kuwa alikuwa anashangiliwa sana alipokuwa anapanda jukwaani.

Sasa mbona stori ipo miguu juu kichwa chini wajameni? au macho yangu?

Hata mimi nashinwa kuielewa, mara amejiondioa, mara alishiriki na alikuwa miongoni mwa kumi bora. Sasa ukweli ni upi??
 
Back
Top Bottom