Mrembo hajui kumuandaa kuku

Mimi kuna mmoja alitumia Unga wa ngano kupika ugali akidhani kuwa ni unga wa sembe.

Na kitu ambacho nilishindwa kuamini alipika kabisa. Haya mambo haya aisee

alikupkia ugali wa kwetu makete mtam sana huo ugali
 
Jamaa yuko right amtafutie tu kisa wanalizane
 
Wanaume wengine hata kuku mwenyewe kumuandaa na kumgawa vipande hawajui. Mifano ipo. Hatupendagi ujinga siye. Ngoma drooo. Yaani hata boxer kufua ni matata hapo mnasemaje? Yaani it plays both ways kama Mzazi hujasimama imara kulea Watoto kujitegemea. Endekezeni Kuwatumikisha ma house boy and girls na mtavuna. Mtu zima hata shoe shine kiatu chake na kupasi mzigo. Eti anasubiria akioa mke awe punda, ngamia, kihongo na tractor la kumfanyia Kazi. Khaaaaaa bora ubaki kwenu uendelee kulelewa na mamako tu.
 
Jamaa yuko right amtafutie tu kisa wanalizane
Aiseee na wanaume wanaosoma magazeti na kukodolea macho vituo vyite vya tv vya mioira na muereka nyumbani wakitumia wake zao kama tractor la Kubota, ngamia na punda itabidi kumalizana haraka zaidi.
 
Hii imenifundisha story moja wakati tunakuwa, baba mmoja jirani yetu alikwenda Egypt kusomea medicine, kula alikutana na binti wa Kiegypt na walioana na kupata watoto, ile family tuliishi nayo mtaani lakini familia ya baba na mama wote madaktari, watoto walikuwa ni kusoma tu, hata kuwe na birthday mtaani hatukuwaona.

Basi yule binti alipata mchumba kijana wa kiarabu, kwao walikuwa na mali, lakini familia yote waliishi nyumba moja. Baada ya harusi na honeymoon ndiyo maisha ya ndoa yalianza pale, walipewa chumba chao self contained. Kupika wanawake ndiyo wapishi, kuanzia mke wa kaka mkubwa mpaka wa mdogo. Chai yao ilinywewa saa nne asubuhi, maandazi ya chai yanaanza kukandwa saa moja na jogoo anataarishwa kila asubuhi.

Ilipofika zamu ya jirani yangu sasa, amewekewa unga akande maandazi na kuku amechinjwa, wakwe, mawifi, mashemeji, wake wenza wanasuburi chai, walipoona vinachelewa walikwenda jikoni, kukuta jogoo ameshaiva kwenye maji yaliyochemshwa kwa kukunyonyolea kuku.
 
Umenikumbusha my best friend
Yeye aliwahi kunambia hawezi kumuandaa kuku kwenye kumnyonyoa kuku anaweza ila kwenye suala la kumtoa utumbo na kumkatakata hawezi.Ikifikaga hatua hiyo mamake au mdogo wake wa kiume anashughulika mana yeye hawezi.
Hajui kabisa kupika chapati wala maandazi na yupo comfortable kabisa wala hajishughulishi ajue.
Sasa hivi ni mke wa mtu nadhani atajifunza.
Malezi ndo yanachangia mtu kuwa hivo.
Kuna vitu unapofanya ndo unajifunza hivo kama hufanyi au hata kutaka kujaribu hutokaa ujue.
 
Mwanamke ambaye hajui kupika apite kuleee! Yani kupika hajui na hela anaomba,, shwainn!!
"the way to a man's heart is through his stomach", endeleeni na undezi tu!
 
AHAHAAA HAJUI KUMFANYIA KUKU OPERESHENI KAKATIA HUMO HADI UTUMBO NA MAVI YAKE
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…