Hii imenifundisha story moja wakati tunakuwa, baba mmoja jirani yetu alikwenda Egypt kusomea medicine, kula alikutana na binti wa Kiegypt na walioana na kupata watoto, ile family tuliishi nayo mtaani lakini familia ya baba na mama wote madaktari, watoto walikuwa ni kusoma tu, hata kuwe na birthday mtaani hatukuwaona.
Basi yule binti alipata mchumba kijana wa kiarabu, kwao walikuwa na mali, lakini familia yote waliishi nyumba moja. Baada ya harusi na honeymoon ndiyo maisha ya ndoa yalianza pale, walipewa chumba chao self contained. Kupika wanawake ndiyo wapishi, kuanzia mke wa kaka mkubwa mpaka wa mdogo. Chai yao ilinywewa saa nne asubuhi, maandazi ya chai yanaanza kukandwa saa moja na jogoo anataarishwa kila asubuhi.
Ilipofika zamu ya jirani yangu sasa, amewekewa unga akande maandazi na kuku amechinjwa, wakwe, mawifi, mashemeji, wake wenza wanasuburi chai, walipoona vinachelewa walikwenda jikoni, kukuta jogoo ameshaiva kwenye maji yaliyochemshwa kwa kukunyonyolea kuku.