Heshima Mkuu,
Saint Ivuga .
FYI anaye-present HARDtalk ( A current affairs interview programme on BBC World News) ni Stephen Sackur na sivyo kama ulivyomuandika. Huyu Steven tucker ni mwingine kabisa,
www.tuckermedical.com/about-dr-steven-tucker/.
Back to the topic, hatuna skills japo a, b, c's za uulizaji wa maswali. Kuna baadhi ya maswali ukiulizwa ni faida kwa umma tulio wengi haswa ikiwa muuliza maswali na mjibu maswali wataongozwa na mantiki. Huku ndiko kufikiri kwa misingi ya dhana.
I think, kwa hapo nyuma
STUNTER aliwahi kum-interview
Nyani Ngabu . Kupitia maswali na majibu ya NN nilijifunza mengi. Tujifunze kutokana na wenzetu, hii ndiyo nidhamu ya kiakili. Na nidhamu kwa lugha rahisi yamaanisha kujifunza.
Pia
FaizaFoxy ana darasa lake,
Faidika na darsa la FaizaFoxy; Uliza chochote utajibiwa, huku pia tulizidi kudhihirisha unazi wetu kwa kuuliza maswali ya hovyo (Kumradhi). Then back the stage tukielezwa ukweli tunang'aka. Kutambua ujinga wetu ni hatua muhimu ya awali ya kujifunza.
Nakubali kupishana kimawazo na ndiyo maisha. Mwenzio akikuzidi shukuru na ujifunze kwake. Ukiona mwenzio uelewa wake uko chini au misimamo yake inachanganya basi mvumilie na jaribu ku-balance kwa kujadili naye kwa hekima.
Kama sisi binadamu ni viumbe wenye akili, matendo yetu lazima yalingane na maumbile yetu. Hivyo vitendo vyetu vinakuwa vitendo vya kiakili, na kwa msingi huo hutupasa kutenda kitu chochote kulingana na maumbile yetu. Hivyo kusema kuwa binadamu ni kiumbe mwenye akili ni karibu na kusema kuwa binadamu yampasa kutenda matendo ya kiakili.
Kumradhi kwa niliowataja kwa upuuzi huu, pia heshima tele kwa
Maserati .
Asalaam.