SI KWELI PreGE2025 Mrisho Gambo anaungana na Luhaga Mpina 'Arusha Oktoba tutalinda kura'

SI KWELI PreGE2025 Mrisho Gambo anaungana na Luhaga Mpina 'Arusha Oktoba tutalinda kura'

Baada ya kuitathmini taarifa hii, tumebaini kuwa si ya kweli.
Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla)
GAMBO16AG2025.jpg
 
Tunachokijua
Mrisho Gambo ni mbunge wa Arusha mjini anayemaliza muda wake ambaye alichaguliwa kuwa mbunge wa jimbo hilo mwaka 2020. Aidha mwaka 2025 Gambo alikuwa ni miongoni mwa watia nia wa ubunge kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM), hata hivyo hakufanikiwa kupenya katika mchujo wa kamati kuu ya Chama hicho baada ya jina lake kutokutangazwa na kamati hiyo Julai 29, 2025

Kumekuwepo na Picha yenye ujumbe unaoonekana kuchapishwa na Mrisho Gambo kwenye mtandao wa X ukisema 'Nimemskiliza Askofu Gwajima na kwa maslahi mapana ya wana Arusha naungana na Mpina. ARUSHA OKTOBA tutalinda kura.'

Je, ni upi uhalisia wa ujumbe huo?

Ufuatiliaji wa kimtandao uliofanywa na JamiiCheck kwa kutumia utafutaji wa maneno muhimu (Key words search) umejiridhisha kuwa ujumbe huo haujachapishwa kwenye ukurasa rasmi wa Mrisho Gambo kupitia mtandao wa X bali ni wa kutengenezwa na wapotoshaji.

Akizungumza na JamiiCheck, Gambo amebainisha kuwa hahusiki na Taarifa hiyo, na alipoulizwa kuhusu mipango yake kuelekea Uchaguzi, amesema kwa sasa hayupo tayari kuongelea masuala ya Uchaguzi kwani yupo mapumziko na anatumia muda wake kuwa karibu na familia​
mama kizimkazi kama atashinda uchaguzi. Ampe gambo ukuu wa mkoa Arusha. zam Kwa zam
 
Back
Top Bottom