Mrisho Gambo ataka Bunge liahirishwe, kujadili mfumuko wa bei

Mrisho Gambo ataka Bunge liahirishwe, kujadili mfumuko wa bei

Hilo bunge lingekuwa na maana kama lingeahirishwa ili kuijadili hiyo hoja na kutoa maelezo kwa serikali nini wafanye kukabiliana na hilo tatizo.

Lakini kama Spika wa bunge alishasema serikali hailazimishwi kufuata ushauri wa bunge, sioni sababu kwanini bunge liahirishwe ili kujadili mfumuko wa bei.

Naona watakuwa wanapoteza muda tu, bora waendelee na mambo yao kama kawaida.
 
suluhisho kwenye ishu ya mafuta Shabiby ameongelea swala la waagizaji binafsi, nikamwelewa. Hio habari iko You tube.


Yesu ni Bwana
 
MaCCM yakiucheza wimbo wa 'Mama anaupiga mwingi'😁😁😁
 
CHAWA huyu anaupiga mwingi sana kwakweli, kwa niaba ya wa-TZ wezangu wote mliopo ndani na nnje ya JF, napendekeza awe anapewa kipato kikubwa sana kuliko CHAWA wengine wote [emoji87]
Sio tuu kuupiga bali kiuvumisha mwingi.

Back kwenye hoja,Wachangiaji wengi Bungeni nimewafuatilia akiwemo Msukuma wameunga mkono hoja ya kuruhusu watu binafsi walete mafuta bei zitashuka.

Pili ametoa ushauri kwa Serikali kwamba ikiwezekana waje na mswaada wa dharura wajadili ima wakope pesa au wapunguze pesa kwenye maeneo mengine Ili watoe ruzuku kwenye mafuta bei zishuke..

Mwisho amemkubali Sana mama Kwa kuupiga mwingi sana na amemalizana na ishu ya kumshambilia Makamba Kuhusu Bwawa la umeme baada ya kufanya ziara mara 4 na kujua ukweli..

Kana kwamba haitoshi amekiri kwamba pesa ni mingi Sana huko majimboni kikubwa usimamizi uongezwe..

Kama Msukuma amekili wewe ni nani hadi umpinge mama?
 
Walioweka tozo ya 300 kwenye mafuta s hao hao wabunge?
Anatufanya sisi mazuzu!
 
Mbunge wa Arusha Mjini, Mrisho Gambo leo Ijumaa Aprili 8, 2022 ametoa hoja akitaka bunge liahirishe shughuli zake ili wabunge wajadili kwa kina kuhusu upandaji wa bei za bidhaa nchini ikiwemo vyakula na vifaa vya ujenzi.
Hilo Bunge limekosa uhalali Maana Wabunge Karibia wote walipita Kwa Wizi, Hila na Ghiliba za Mwendakuzimu
 
Kweli mkuu maana hakuna asiyejua kwamba kuna mfumuko wa Bei sio tuu Tanzania bali Dunia yote na sababu zinafahamika..

Pili mfumuko wa bei kwa Tzn imeshuka kidogo kutoka 4.2 mwezi Desemba hadi 3.7 mwezi machi..

Mfano bando ya Bati za rangi imepungua kutoka 459,000 mwezi tajwa hadi wastani wa 432,000 kwa sasa..

Kwenye vyakula bei zitazidi kupungua kwa sababu tunaelekea msimu wa mavuno,walo mikoa ya Nyanda za Juu Kusini ni mashahidi kwamba Bei za vyakula zimeanza kupungua.
sana maharage kilo ni buku mahindi gunia 2700 la kilo mia,mafuta ya kula lita 2500 huku kusini tuna neema sana na vyote hivyo havina soko mpaka unagawa bure
 
sana maharage kilo ni buku mahindi gunia 2700 la kilo mia,mafuta ya kula lita 2500 huku kusini tuna neema sana na vyote hivyo havina soko mpaka unagawa bure
Ila hizi bei zinaumiza Sana Wakulima,wanahangaika afu vitu vikipanda kidogo watu waliovimbiwa kutoka mjini wanakuja kupiga makelele ya kipuuzi.

Aisee huwa nasikitika Sana
 
Back
Top Bottom