Pre GE2025 Mrisho Gambo: Nitaenda kuwajibu nini wananchi wa Arusha. Jiji kama Arusha linakosaje stendi?

Pre GE2025 Mrisho Gambo: Nitaenda kuwajibu nini wananchi wa Arusha. Jiji kama Arusha linakosaje stendi?

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla, wakati na baada)
Gambo ndiye chanzo kutofanyika kwa ujenzi wa hiyo stendi alafu ananyoosha kidole kwa nani?.

Wakati wa JPM pesa ilitolewa, eneo lilishapimwa na mpaka mkandarasi alishasafisha eneo, baadaye wakaanzisha mtifuano kwamba kule mbali, kumbe Gambo and Company wanataka stand ijengwe kwenye eneo lao.

Mzee baba akaona hawa hawaitaji stand, pia soma hii; Kituo Chetu Mabasi Arusha hiki hapa
Well said. Nilitaka niandike hicho hicho.
Huyo mpiga dili ni mnafiki na dumilakuwili pia
 
Geneva ya Africa bado wanatumia stand ya mwaka 47
Actually bus stand si dili sana Tanzania. Mengi yamejengwa lakini hayana faida wala huduma za msingi!
Labda wanaotaka stand mpya watumie hoja ya kuupanua mji wa Arusha usambae hadi Kisongo, Ngaramtoni ya Juu, Lokii/Custom, King'ori, etc
 
Standa ya Arusha ni mfupa mgumu, wengi wamejaribu wameshindwa.
Viwanja vimetolewa mara 3 lkn mradi umekwamishwa na vigogo.

Hili lilimshinda hadi Magufuli.
Arusha ina wenyewe.
Mafisadi ya nchi hii yananufaika kwa mkwamo wa stand kuu.

Hata Magufuli alikwama
Kinachikwamisha ni siasa za ccm duni za ongeza na thamani ya kubwa ya ardhi.
Lakini hoja ya kupeleka bus terminal kule Bondeni City haitokuwa na faida kama hakutakuwa na terminal nyingine barabara ya Nairobi (Ngaramtoni ya Juu), barabara ya Babati (Kisongo) na barabara ya Moshi (Usa River)!
Bondeni City imekaa kushoto sana na itawanufaisha zaidi watumiaji wa barabara pendekezwa ya Arusha-Dodoma!
Waendelee kuumiza vichwa!
 
Back
Top Bottom