Mrisho Mpoto: Mr. Blue ndiye msanii bora Tanzania

Mrisho Mpoto: Mr. Blue ndiye msanii bora Tanzania

chinchilla coat

JF-Expert Member
Joined
May 16, 2016
Posts
5,107
Reaction score
10,969
x14240737_1128283583922262_1534775813_n.jpg.pagespeed.ic.Rg33h2XObj.jpg

Kwa mujibu wa Mrisho Mpoto, Harry Sameer, wamjua zaidi kama Mr Blue, anastahili kuwa msanii bora Tanzania.
Mpoto alidiriki kusema hivyo baada ya kushuhudia show ya hitmaker huyo wa ‘Mboga Saba’ akitumbuiza kwenye Fiesta mjini Shinyanga na kudai kuwa hajawahi kuona show moto kama ile.

“Naomba leo niseme kwa mara ya kwanza kwamba Mr Blue anastahili kuwa msanii bora katika nchi yetu ya Tanzania,” alisema Mpoto kwenye promo ya show hiyo iliyoruka Clouds FM.

Kwa miaka mingi Mr Blue amekuwa akisifiwa kwa uwezo mkubwa wa kutumbuiza jukwaani. Mwaka juzi wakati wa show hiyo pia, Kabayser alitajwa na waandaji wa Fiesta kuwa msanii aliyepata shangwe kuliko wote. Kipindi hicho alikuwa akihit na wimbo wake Pesa.

Kwa sasa Blue anafanya vizuri na wimbo wake ‘Mboga Saba’ aliomshirikisha Alikiba.

Chanzo: Bongo 5
 
No doubt ni moja ya legends wa bongo flavor, very influential, muasisi wa mikato fulani ya kipekee kwenye tasnia, kadumu kwenye game for quite some time na moja ya msanii anayependwa sana sio rahisi kumkuta mtu hamkubali blue.
 
mtu akitembea peku lazima atakau ana matatizo ya saikolojia

labda anajifanya kipofu hamuoni plutnumz
labda anajitia ukiziwi hamsikii domo
labda amejitoa ufahamu kwa mafanikio ya domo
 
Ni mtazamo wake,kama yule msanii wa Nigeria Kiss Daniel aliposema,Harmonize ni msanii bora kwa TZ.
 
mtu akitembea peku lazima atakau ana matatizo ya saikolojia

labda anajifanya kipofu hamuoni plutnumz
labda anajitia ukiziwi hamsikii domo
labda amejitoa ufahamu kwa mafanikio ya domo

Mkuu hizo ni business strategy, lazima wasanii walioko kwenye timu ya Fiesta wasifiwe kwamba wao ndio wasanii bora kabisa ili viingilio viwe vingi, huyu kaambiwe aseme hivyo.
 
Watu huwa wanaota wakiwa usingizini,jamaa anaota akiwa macho
 
Hivi Shilole hayupo kwenye Fiesta ya mwaka huu?
 
Bongo mwanamuziki wangu ni Ben Pol. namkubali sana.
 
Mkuu hizo ni business strategy, lazima wasanii walioko kwenye timu ya Fiesta wasifiwe kwamba wao ndio wasanii bora kabisa ili viingilio viwe vingi, huyu kaambiwe aseme hivyo.
mitazamo ya hovyo hovyo na kama kaambiwa basi aliyemwambia ni mtu wa hovyo hovyo
 
mitazamo ya hovyo hovyo na kama kaambiwa basi aliyemwambia ni mtu wa hovyo hovyo

Wanataka ionekane kwamba Fiesta Team ina msanii ambaye ni bora Tanzania, kwa hiyo watu waende kumwona msanii bora kuliko wote Tanzania.
 
Wanataka ionekane kwamba Fiesta Team ina msanii ambaye ni bora Tanzania, kwa hiyo watu waende kumwona msanii bora kuliko wote Tanzania.
tatizo ni hiki kizazi hatutaki kuaminishwa vitu vya hovyo hovyo
 
Back
Top Bottom