Mrithi wa Lewis Hamilton, Kimi Antonelli, anawapelekea moto wakongwe kwenye F1 Championship. Dogo atafika mbali!

Mad Max

JF-Expert Member
Joined
Oct 21, 2010
Posts
35,566
Reaction score
104,386
Baada ya Lewis Hamilton kuhama Mercedes Benz na kwenda Ferrari wengi tulitegemea maajabu mengi ila hamna kitu. Ata podiums tu huu msimu za kuhesabika.

Move ya MB kumtoa Kimi Antonelli kutoka Mercedes Benz Junior Racing kuja F1 kumreplace Hamilton wengi walijua wamebugi. Ila dogo ni wa moto.

Akiwa na miaka 19 tu, miaka ambayo huku kwetu mtu bado yupo A-Level, dogo ameshashika podiums 3, fastest rap 3 na yupo nafasi ya 7 katika msimamo wa F1 Driver Championship akiwa na point 137.

Leo kwenye Las Vegas GP kaonesha balaa kutokea nafasi ya 17 kusogea hadi nafasi ya 3 baada ya race kuisha. Ni kama 2021 Max alivotoka namba 17 hadi akaja kushika namba 1. Sio poa aisee.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…