Mrusi alituambia mara hii hakutakuwa na kombe la dunia imekuwaje tena?

Mrusi alituambia mara hii hakutakuwa na kombe la dunia imekuwaje tena?

5525

JF-Expert Member
Joined
Apr 6, 2014
Posts
5,412
Reaction score
6,279
Ndivyo tulivyokuwa tunapeana habari baada ya timu ya Russia kuondolewa kwenye mashindano hayo kwa kosa la kuivamia Ukraine Kijeshi, kwamba rais Putin ametangaza kuwa hakutakuwa na kombe la dunia kwa vile timu yake imeondolewa ikitafsiriwa Urusi itapeleka mashambulizi huko Qatar ili shughuli za kombe la dunia zifeli mpaka pale timu ya Taifa ya Russia nayo itakaposhiriki.

Naleta kwenu wadau kwa uchambuzi na ukweli wa kauli hii Je Rais Putini alitamka kweli? na kama alitamka ni kwanini sasa kombe la dunia linaendelea kuchezwa kwa shangwe na hoi hoi nchini Qatar ambapo jana mwenyeji alilala 2 kwa sufuri.
 
Na inavyoonekana Russia na michezo ni baibai labda Putin aondoke madarakani na kwa namna hii hata michezo ya ndani tu huko Russia haina maana kabisa watazidiwa hata na DPRK ya Kiduku.
 
Back
Top Bottom