Msaada: Alieniuzia kiwanja kisicho chake ananikana kutonijua

Msaada: Alieniuzia kiwanja kisicho chake ananikana kutonijua

Going Concern

JF-Expert Member
Joined
Jul 25, 2011
Posts
1,071
Reaction score
1,212
Kuna mtu aliniuzia kiwanja nikafata taratibu zote kama kupitia kwa mwenyekiti wa mtaa....na Afisa mtendaji, Baadae kufatilia katika kutafuta hati nikaja kugundua kiwanja sio chake,

Nimefungua kesi mahakama ya wilaya, akaitwa... hakimu akasema anaitaji mashaidi, bahati mbaya mtu niliyemtumia kama shaidi yangu yuko mkoani kizazi, hakimu anasema yeye anataka shaidi... ninamikataba yote aliyosaini pamoja na picha zake.... kipi chakufanya nipate haki yangu?
 
Pole mkuu kweli hiyo sio mbopo maana uvamizi wa maeneo umezidi
 
Hayo ni sawa na mambo ya wilaya moja mkoa wa Pwani. Unauziwa kiwanja feki, mwenye kiwanja ni feki, mwenyekiti wa serikali ya mtaa feki, na wakati wa mauziano unaletewa na wazazi wa muuzaji ambao nao ni feki. Pole mkuu!
 
Kiwanja chenye hatimiliki (surveyed plot) hatuandikishani serikali za mtaa, bali kwa mwanasheria ambako unaandaliwa mkataba maalumu ambao unapelekwa ofisi ya ardhi kwa ajiri ya kubadilisha umiliki.
 
Hayo ni sawa na mambo ya wilaya moja mkoa wa Pwani. Unauziwa kiwanja feki, mwenye kiwanja ni feki, mwenyekiti wa serikali ya mtaa feki, na wakati wa mauziano unaletewa na wazazi wa muuzaji ambao nao ni feki. Pole mkuu!
Iweke hadharani kwa faida ya wanajf wote
 
Back
Top Bottom