Msaada: Alinikopesha laki 5 kwa ahadi ya kumrudishia laki 6 kwa maandishi baina yetu, leo kaenda kunishtaki ananidai milioni 1

Jayselejm

New Member
Joined
Feb 22, 2023
Posts
3
Reaction score
12
Kuna mtu aliniazima pesa kiasi cha laki tano nikaelewana nae nitamlipa laki sita lakini mambo hayakuwa sawa nikamuomba kumlipa kidogo kidogo na tuliandikiana kwa karatasi tu kishikai sisi wenyewe wawili.

Lakini leo ameenda nishitaki mahakama ya mwanzo na wameniletea samansi lkn ameandika kuwa ananidai milioni moja.

Hii imekaaje?
 
Aonyeshe mahakamani iyo leseni ya taasisi yake ya ukopeshaji kwa riba
 
Lipa tu deni ndugu hamna jinsi humu hamna msaada watakulisha matangopori
 
Mkitska kukopa mtujuze pia sio kinawashika shingon mnatuhusisha
 
Mnavyotukopa maneno mengii yenye busara kurudisha sasa
mimi kuna coworker idara tofauti taasisi moja nilimdhamini kwq hao wqnokopesha kwa riba kwa mwezi.Huyu anayekopesha nafahamiana naye .Huyu coworker baada ya kupata pesa akaanza kuzingua kulipa miezi inakatika anapiga danadana ilipofika miezi 4 nikaenda kushitaki kwa incharge wake wa idara nikakuta incharge na coworkers wengine pia wanamdai na kulipa kawazingua,nikaenda kwa mkuu wake wa idara akasema hata yeye alishamuazima hakumrudishia.Nikaenda kwa HR nikakuta kuna foleni ya wanaomdai ambapo kuna posho ndani zikiingia huwa zinakatwa juu kwa juu kulipa madeni.Nikaenda mahakama ya mwanzo,nikashinda kesi akamriwa alipe.Baadae nikaona usumbufu kufuatilia kesi nikaamua kupotezea.Baada ya kuona kimya simfuatili akawaambia coworkers wengine ambao wanatakiwa warejeshe kwa yule anayekopesha ninayefahamiana naye ,kuwa hata wao wasilipe deni kwa vile hakuna ambacho tunaweza kufanya wakienda mahakamani huwezi kulipa deni au utawaambia mahakama nitakuwa nalipa kidogokidogo hata buku buku kila mwezi,halafunkesi ya madai haina uzito nyie msilipe mbon yeye amekopa na hakalipa na hata tulipompeleka mahakamani hakuna alicholipiswa.Basi yule mkopeshaji akanilalamikia yule mtu wako uliyemzamini akadhulumu pesa sasa anashawishi na wwngine wasilpe.
NIKAAMUA KUKOMAA NA KESI mwisho wa siku mshahara wake tuliuzuia ikawa hawezi kutoa pesa kwq njia ya mobile sim banking,hawezi kutoa kwa njia ya ndani,mpaka deni alilokopa likarejeshwa ndipo akaunti ikafunguliwa.Kuna watu wana tabia ya kukopa kwa lengo la kidhulumu wenzao,japo sio wote.Nashauri tuwe waaminifu tukikopa hela ikakusaidia kutatua changamoto zako au kama ulizitumia kwq anasa zako starehe zako ukumbuke kirudisha.1)kukopa harusi kulipa matanga
2)usiku wa deni haikawii kukucha
3)dawa ya deni ni kulipa
Hata benki tu zinakopesha kwa riba,wewe unapokopeshwq hela siyo kwamba anayekuopa pesa yeye ni mjinga au hana kazi nazo au anagawq bure au ameokota au amechuma kwwnye mti au amechimba chini.
TUWE WAINGWANA kuanza kupekekana kwenye vyombo vya sheria sijua mahakamani wakati sio fresh kabisa.
dedication
NILIPE NISEPE by belly nine
 
Muache akushtaki.

Hiyo kesi umeshashinda kabla hata haijaanza.

Mtu yeyote haruhusiwi kukopesha kwa riba bila leseni ya Bank of Tanzania
 
Maana yake umekiuka makubariano. Imeenda imetengeneza liba mpaka kufikia huko kwa hesabu zile zile mlizoandikishana. Tatizo Mbongo ukimuazima tu hela kurudisha ni tatizo.
 
Mbona Kuna Vitu mlikubaliana na hujasema!?
 
Kuna mtu aliniazima pesa kiasi cha laki tano nikaelewana nae nitamlipa laki sita lakini mambo hayakuwa sawa nikamuomba kumlipa kidogo kidogo na tuliandikiana kwa karatasi tu kishikai sisi wenyewe wawili.
Ilikuwa irudi baada ya muda gani mlivyoahidiana.

Utashauriwa kuwa kisheria nk unatoboa (mfano haruhusiwi kudai riba kama hajasajiliwa BOT). Lakini kabla hatujafika huko tukuulize wewe je? Umetimiza/unatimiza mambo yote mliyokubaliana na huyo rafiki yako?
 
Maana yake umekiuka makubariano. Imeenda imetengeneza liba mpaka kufikia huko kwa hesabu zile zile mlizoandikishana. Tatizo Mbongo ukimuazima tu hela kurudisha ni tatizo.
We nae hujui sheria, chunga sana usije ukaumia, ni kosa kisheria kukopesha kwa riba bila leseni kutoka bot, sasa hao wote wanaokopeshana kwa kuandikishana ni kazi bure siku mambo yakiharibika usije ukaenda kokote kushtaki kwasababu hio kesi inakugeukia na hautolipwa, hapo jamaa kashashinda kesi kabla haijaanza 🙂
 
Ni kosa kisheria kukopesha kwa riba bila leseni kutoka bot, sasa hao wote wanaokopeshana kwa kuandikishana ni kazi bure siku mambo yakiharibika usije ukaenda kokote kushtaki kwasababu hio kesi inakugeukia na hautolipwa, hapo jamaa kashashinda kesi kabla haijaanza 🙂
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…