Mnavyotukopa maneno mengii yenye busara kurudisha sasa
mimi kuna coworker idara tofauti taasisi moja nilimdhamini kwq hao wqnokopesha kwa riba kwa mwezi.Huyu anayekopesha nafahamiana naye .Huyu coworker baada ya kupata pesa akaanza kuzingua kulipa miezi inakatika anapiga danadana ilipofika miezi 4 nikaenda kushitaki kwa incharge wake wa idara nikakuta incharge na coworkers wengine pia wanamdai na kulipa kawazingua,nikaenda kwa mkuu wake wa idara akasema hata yeye alishamuazima hakumrudishia.Nikaenda kwa HR nikakuta kuna foleni ya wanaomdai ambapo kuna posho ndani zikiingia huwa zinakatwa juu kwa juu kulipa madeni.Nikaenda mahakama ya mwanzo,nikashinda kesi akamriwa alipe.Baadae nikaona usumbufu kufuatilia kesi nikaamua kupotezea.Baada ya kuona kimya simfuatili akawaambia coworkers wengine ambao wanatakiwa warejeshe kwa yule anayekopesha ninayefahamiana naye ,kuwa hata wao wasilipe deni kwa vile hakuna ambacho tunaweza kufanya wakienda mahakamani huwezi kulipa deni au utawaambia mahakama nitakuwa nalipa kidogokidogo hata buku buku kila mwezi,halafunkesi ya madai haina uzito nyie msilipe mbon yeye amekopa na hakalipa na hata tulipompeleka mahakamani hakuna alicholipiswa.Basi yule mkopeshaji akanilalamikia yule mtu wako uliyemzamini akadhulumu pesa sasa anashawishi na wwngine wasilpe.
NIKAAMUA KUKOMAA NA KESI mwisho wa siku mshahara wake tuliuzuia ikawa hawezi kutoa pesa kwq njia ya mobile sim banking,hawezi kutoa kwa njia ya ndani,mpaka deni alilokopa likarejeshwa ndipo akaunti ikafunguliwa.Kuna watu wana tabia ya kukopa kwa lengo la kidhulumu wenzao,japo sio wote.Nashauri tuwe waaminifu tukikopa hela ikakusaidia kutatua changamoto zako au kama ulizitumia kwq anasa zako starehe zako ukumbuke kirudisha.1)kukopa harusi kulipa matanga
2)usiku wa deni haikawii kukucha
3)dawa ya deni ni kulipa
Hata benki tu zinakopesha kwa riba,wewe unapokopeshwq hela siyo kwamba anayekuopa pesa yeye ni mjinga au hana kazi nazo au anagawq bure au ameokota au amechuma kwwnye mti au amechimba chini.
TUWE WAINGWANA kuanza kupekekana kwenye vyombo vya sheria sijua mahakamani wakati sio fresh kabisa.
dedication
NILIPE NISEPE by belly nine