Superb2014
JF-Expert Member
- Jul 29, 2017
- 9,266
- 7,426
Inahuzunisha sana.
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
"WEMA NA UBAYA, VYOTE NI MADENI"Nipo kwenye mahusiano na huyu Dada kwa mwaka mmoja na nusu sasa. Hatuishi pamoja lakini muda mwingi nipo kwake, ananihudumia kwa kila kitu. Mimi nafanya kazi lakini kipato changu ni kidogo sana siwezi kuhudumia mwanamke nayeye anajua. Amenilipia kodi kwenye nyumba nzuri, kaninunulia Pikipiki na kila mahitaji yangu yote.
Namshukuru Mungu kwa hilo, wakati naanzisha naye mahusiano nilimuambia kuwa nina mwanamke wangu ambaye yuko mkoa mwingine na anajua tunawasiliana naye. Hakuonekana kuwa na shida na hilo lakini kadri siku zinavyoenda niliona anazidisha wivu hataki niwasiliane na huyo mwanamke, alikua ananibana sana kuna kipindi akamblock mwanamke wangu kwenye simu yangu.
Nilitafuta namba nyingine na kumuambia Mpenzi wangu kuwa ile namba yangu nilipoteza na Voda wakaigawa hivyo asiipige na kweli nikawa nawasiliana naye kimyakimya mpaka sasa. Sababu ya kuja kwako ni hivi, huyu dada alikua analazimishia sana nimbebeshe mimba, mimi nilikua nakwepa sana lakini kama unavyojua haya mambo ukitengewa chakula unakula, ana mimba yangu.
Amelazimisha sana niende kujitambulisha kwao na kutoa mahari lakini nilikua nakataa, alinipa milioni mbili ili kwenda kutoa mahari kwao, nilienda hivyo hivyo nikajitambulisha kwao lakini sikutoa mahari nilimuambia bado mpaka kwetu wajipange kwani Baba alikua anaumwa.
Baada ya kuona kuwa ananisumbua Nilijiona kama mimi ndiyo mwanamke kwake, nilichukua ile milioni mbili, nikaenda kwa mpenzi wangu, nikatoa mahari nusu na kuwaambia kuwa nataka kufunga ndoa ya harakaharaka nimefunga ndoa ya kanisani ilke ya suabuhi tun a watu wachache. Sababu ya kuja kwako ni hivi, namuachaje huyu dada bila kumuumiza kwani pamoja na kwamba ana wivu sana na ni king’ang’anizi sana lakini hajawahi kunifanyia kitu kibaya.
Mjinga kweliWewe ni mjinga, ushafanya maamuzi hapa unakuja kuuliza nini sasa
🤣🤣🤣🤣View attachment 3081926Usije ukarudi hapa unalia atakapokata msaada!
Tena asubiri kwa upole kabisa pasipo kuhangaika.Ngoja ulogwe😂😂