Msaada anayejua namna ya kudhibiti wizi wa mifugo shambani

Bahatinasibu

Member
Joined
Oct 22, 2021
Posts
73
Reaction score
77
Kama kichwa cha habari kinavyosema naomba kufahamishwa mbinu mbalimbali za kudhibiti wezi wa mifugo shambani.
 
Mifugo aina gani mkuu? Maana kila mfugo una aina yake ya uibwaji mathalani hawawezi beba ng'ombe mgongoni etc.

Ila unaweza changanya mifugo yako na kanga au kuku wa kutosha. Hao ndugu akiingia mtu na akagusa gusa ile huwa wanapiga kelele hadi majirani wanaweza kuja kuona shida ipo wapi.
 
Nafuga mbuzi na kuku ila majirani wanaibiwa sasa nilikua nafikiri kuweka mlinzi ila sasa bado haijafikia kunilipa ndo maana nikaomba ushauri. Kuweka mlinzi kwa sasa itakuwa gharama.

Kuku ni wa kienyeji wapo kama kumi na saba pamoja na wadogowadogo, mbuzi ninao 10 tu watatu kati ya hao 10 ni wadogo
 
Watenge kwenye eneo dogo karibu na nyumba ya wafanyakazi..!weka fensi ya waya huku ukijipanga kupanda michongoma katika eneo lako..!inaweza kusaidia kidogo..!pia weka mbwa karibu na eneo ulilowatenga na liwe karibu na nyumba..!
 
Nafuga mbuzi na kuku ila majirani wanaibiwa sasa nilikua nafikiri kuweka mlinzi ila sasa bado haijafikia kunilipa ndo maana nikaomba ushauri. Kuweka mlinzi kwa sasa itakuwa gharama.

Kuku ni wa kienyeji wapo kama kumi na saba pamoja na wadogowadogo, mbuzi ninao 10 tu watatu kati ya hao 10 ni wadogo
Tafuta mbwa wazuri wa2 wafuge. Hakuna kenge atakae sogelea shamba lako...
 
Ukiweka mbwa makenge watakuja na nyama yeye sumu watampa mbwa atakufa papo hapo na wataiba mifugo yako kirahisi... Mi vyema ukafunga alarms system ambayo itakuwa inatoa taarifa iwapo watu watasogelea makazi ya mifugo yako.
Ndugu hii si ni gharama sana?
 
Ukiweka mbwa makenge watakuja na nyama yeye sumu watampa mbwa atakufa papo hapo na wataiba mifugo yako kirahisi... Mi vyema ukafunga alarms system ambayo itakuwa inatoa taarifa iwapo watu watasogelea makazi ya mifugo yako.
Mbwa ukiwafuga huwa tunawafunguwa kwa zamu huruhusiwi kufungua Mbwa kwa pamoja na uwazoweshe Mbwa wako kulia ndani ya mabanda yao, Mbwa ni suluhisho kubwa sana ktkt ulinzi, pia usizoeshe watu wengi kila mara kusogelea mabanda yako na kuona mwenendo wa ufugaji wako kwa ndani.
 
Kwa kweli umenifungua macho, ntalifanyia kazi hili
 
Nafuga mbuzi na kuku ila majirani wanaibiwa sasa nilikua nafikiri kuweka mlinzi ila sasa bado haijafikia kunilipa ndo maana nikaomba ushauri. Kuweka mlinzi kwa sasa itakuwa gharama.

Kuku ni wa kienyeji wapo kama kumi na saba pamoja na wadogowadogo, mbuzi ninao 10 tu watatu kati ya hao 10 ni wadogo
Zungushia fensi uwe
 
Ukipata hela tafuta kitu unaitwa stun gun mlinzi akae nacho. Mwizi hata awe baunsa atakua neutralized. Hii kitu inapiga short ya umeme kwa mlengwa mpaka anajikojolea. Benson Arusha walikua Nazi lakin nasikia container ilippkuja ya pili ikazuwiliwa bandarini. Lakin unaweza kuagiza mwenyewe
 
Back
Top Bottom