Msaada: Anayeweza kuniunganisha na masoko ya mbao DSM bila dalali

Msaada: Anayeweza kuniunganisha na masoko ya mbao DSM bila dalali

Mkuu, sina hoja inayoendana na swali lako ila ningeomba kukuuliza swali. Kule mafinga ninaweza kupata miti ya cypress kwa wingi?
Hii miti haioteshwi sana ila kuna uncle wangu ana kama around eka 5 Kijiji kinaitwa Usokami. Kama inakufaa nikuunganishe naye.
 
Kwa uzoefu kidogo nilio nao wa Mufindi, cyprus ni miti adimu mno, shamba kubwa lipo karibu na kijiji cha Nundu ni la SAO HILL. Watu binafsi hawaoteshi Cyprus, hata ukiiona sehemu, basi ni ya taasisi kama makanisa au shule au familia bora.

Kwa kuokoteza nenda kijiji cha Ng`ang`ange wilaya ya Kilolo Iringa karibu na Boma Ng`ombe, waweza pata miti miwili mitatu hivi.
Kweli miti hii ni shida. Kuna uncle wangu anayo hiyo miti kama acre 5 tu nadhani kijiji kinaitwa Usokami kama sijakosea.
 
Si kweli Mkuu, Mataperi wapo kila sehemu, hata Mikoani ni wengi sana, sema Madalali wengi wa Dar sio Waaminifu, Utaperi ni Fani Mkuu.

Na watu wengi wa Mikoani ni rahisi kutapeliwa kwa sababu ya Tamaa ama Ubinafsi, wakishatapeliwa lawama zote kwa Wakazi wa Dar!

Ni Vile tu mtoa mada hajataka mtu wa kati, ningemuunganisha na soko la Tegeta, Tegeta kuna Soko zuri la Mbao, na Buyers ni really, soko ni kubwa na wanaenda kununua wenyewe Mbao Iringa, wako Buyers wakubwa wanaleta Malori yao wenyewe, pia wapo Buyer wadogo wanachangishana watu kadhaa wanaenda kuleta mzigo!

Sasa kama seller anaweza kuleta mzigo mwenyewe anauza tu Cash na Chap kwa haraka!
Mkuu, kando na Tegeta ni sehumu gani nyingine tena yenye masoko kubwa ya mbao mjini Dar es salaam?
 
Mkuu, kando na Tegeta ni sehumu gani nyingine tena yenye masoko kubwa ya mbao mjini Dar es salaam?
Mazense Darajani mtaa wa nyuma, kuna Viwanda vingi vya Mbao, wananua na kuuza, Tegeta kuna soko kubwa sana la Mbao, Buguruni CCM pia kuna soko kubwa la Mbao, Boko up to Bunju kuna Maduka Makubwa ya Ujenzi yanauza Mbao, maeneo mengi kuna Maduka makubwa ya ujenzi japo hayana Soko kubwa la Mbao kama Tegeta na Buguruni, kuanzia Mbezi ya Kimara mpaka Mbezi CCM huko, Tabata, River side, na Maeneo ya Temeke, Mbagala huko n.k
 
Back
Top Bottom