Msaada: Anayeweza kuniunganisha na masoko ya mbao DSM bila dalali

Mkuu, sina hoja inayoendana na swali lako ila ningeomba kukuuliza swali. Kule mafinga ninaweza kupata miti ya cypress kwa wingi?
Hii miti haioteshwi sana ila kuna uncle wangu ana kama around eka 5 Kijiji kinaitwa Usokami. Kama inakufaa nikuunganishe naye.
 
Kweli miti hii ni shida. Kuna uncle wangu anayo hiyo miti kama acre 5 tu nadhani kijiji kinaitwa Usokami kama sijakosea.
 
Mkuu, kando na Tegeta ni sehumu gani nyingine tena yenye masoko kubwa ya mbao mjini Dar es salaam?
 
Mkuu, kando na Tegeta ni sehumu gani nyingine tena yenye masoko kubwa ya mbao mjini Dar es salaam?
Mazense Darajani mtaa wa nyuma, kuna Viwanda vingi vya Mbao, wananua na kuuza, Tegeta kuna soko kubwa sana la Mbao, Buguruni CCM pia kuna soko kubwa la Mbao, Boko up to Bunju kuna Maduka Makubwa ya Ujenzi yanauza Mbao, maeneo mengi kuna Maduka makubwa ya ujenzi japo hayana Soko kubwa la Mbao kama Tegeta na Buguruni, kuanzia Mbezi ya Kimara mpaka Mbezi CCM huko, Tabata, River side, na Maeneo ya Temeke, Mbagala huko n.k
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…