Kama kichwa cha habari hapo juu kinavyo jieleza wapendwa wangu wana JF wenzangu :
Baba yangu ni mgonjwa yapata miaka mitatu,matibabu amepatiwa bila mafanikio,na anatibiwa kwa kubahatisha kwani ugonjwa haujalikani.
Ugonjwa wake ni kuanguka na kukakamaa mwili huku akisaga meno,tatizo hili humtokea baada ya mwezi au miezi miwili.
Naombeni msaada wenu wa mawazo,ushauri kujua ni tatizo gani au kama kuna mtu alisha wahi uguza mgonjwa wa hivi.
Ni zaidi ya maumivu kwangu kumwona Baba vile nisaidieni Ndugu zangu asanteni.
Pole sana. Yaelekea hizo ni dalili za ugonjwa wa akili na unahitaji mbingwa wa afya ya akili. Mimi kuna kijana nilimsaidia kumpeleka Mirembe na amepata nafuu na hivi sasa ameshaoa pia amebahatika kuwa na familia yake. Hapo awali ilikuwa mtihani sana kwani akiingia kwenye "game" alikuwa anakakamaa. Nakushauri mpeleke Mirembe kuna mabingwa wazuri wa afya ya akili.Ametibiwa hospitali mbalimbali mojawapo ni ikonda tulisikia kuna Huduma nzuri tukampeleka
Yah hicho ni kifafa.Kifafa mkuu hiyo ilimtokeaga dadaake na rafiki yangu na alipona kwa tiba za jadi japo amefariki kwa ugonjwa mwingine kabisa,alikuwa anang'ata na kutafuna hadi mchanga
cc. Mzizi mkavu mshana jr
Mungu akusamehe kwa kuwa hulijui usemaloAcheni utapeli wenu kabisa.uliona wapi maombi ni dawa. Mpeleke hosp akapate tiba sahihi.maombi ni wizi na kumzidishia maumivu mgonjwa
Mkuu kumfuata mtu PM sio kumtapeli, pia sio habari za YESU tu hata habari za waganga zinatangazwa kwenye vipaza sauti.Unampa Habari za Yesu, ila unataka aje sirini! we ni mpuuzi sana, unataka umtapeli?
Mbona habari za Yesu wengine wanazitangaza kwa vipaaza sauti ili kila mtu asikie?
Upo mkoa gani maana mimi nilimtibia iringa ingawa gharama ni kubwa nilifumba macho ukiona bora ni pm au hadharaniUlifanikisheje Mkuu?
Cha kutupiwa ndo maana nikasema maombeziKifafa ukubwani Mkuu 70yr
U.T.A.P.E.L.I.Kuna jamaa yangu mama yake mdogo alikuwa na tatizo kama hilo kalazwa Muhimbili muda pamoja matibabu mengi bado hukupona haraka.
Jamaa zake wakamshauri ampeleke kwenye maombi sasa hivi majuzi namuulizia vipi mgonjwa hali yake ikoje kwa ssa? akanijibu "usicheze na Yesu" baadaye ndo akanipa mkanda mzima kuwa aliombewa akatapika sana mpaka sasa nimzima kabisa!!
Nilitaka kujua ilivyokuwa kwasababu hali ya mgonjwa nilikuwa naifahamu sema tu jamaa alikuwa na haraka ya safari. Baadaye ndo nikampigia simu akanipa mkanda habari ndefu kuhusu maombi.
Alinitajia jina la Mchungaji aliyemuombea kwamba anaitwa PARAPANDA na kwamba yuko Dar es salaam Tanzania . Japokuwa jina lake linatisha ila kwa vile muhusika anadhibitisha mama yake alipona haina shida.Nakushauri nenda Hospitali lakini pia
Mtafte huyu mchungaji
Sema hapahapa ili iwe kwa msanufaa ya wengiNina ndugu yangu alikuaga anatatizo Kama hilo hivyo hivyo ulivyolezea..alizunguka kila hospital na kufanya vipomo vingi Sana baadae akagundulika Ana tatizo na nerves kichwani akapewa dawa za kutumia kwa muda was miaka miwili na kila baada ya miezi 3 anaenda kufanya vipomo miaka miwili inaisha february mwakani na hajawahi kuanguka tena..tuwasiliane labda naweza nikakusaidia hata kwa kukuelekeza ukamuone nani
leta suluhisho basiU.T.A.P.E.L.I.