Msaada: Baba yangu ana tatizo la kuanguka na kukakamaa mwili huku akisaga meno

Msaada: Baba yangu ana tatizo la kuanguka na kukakamaa mwili huku akisaga meno

Kama kichwa cha habari hapo juu kinavyo jieleza wapendwa wangu wana JF wenzangu :

Baba yangu ni mgonjwa yapata miaka mitatu,matibabu amepatiwa bila mafanikio,na anatibiwa kwa kubahatisha kwani ugonjwa haujalikani.

Ugonjwa wake ni kuanguka na kukakamaa mwili huku akisaga meno,tatizo hili humtokea baada ya mwezi au miezi miwili.

Naombeni msaada wenu wa mawazo,ushauri kujua ni tatizo gani au kama kuna mtu alisha wahi uguza mgonjwa wa hivi.

Ni zaidi ya maumivu kwangu kumwona Baba vile nisaidieni Ndugu zangu asanteni.

Kwa bahati mbaya sana Baba anaugua kifafa! Ugonjwa mbaya sana ulimtesa marehemu Mama yangu mpaka nikifikiria dah! Huo ugonjwa unadhalilisha hususani kwenye jamii yetu ilojaa unyanyapaa!

Kama ndo inaanza wahi akapimwe mapema
 
Ametibiwa hospitali mbalimbali mojawapo ni ikonda tulisikia kuna Huduma nzuri tukampeleka
Pole sana. Yaelekea hizo ni dalili za ugonjwa wa akili na unahitaji mbingwa wa afya ya akili. Mimi kuna kijana nilimsaidia kumpeleka Mirembe na amepata nafuu na hivi sasa ameshaoa pia amebahatika kuwa na familia yake. Hapo awali ilikuwa mtihani sana kwani akiingia kwenye "game" alikuwa anakakamaa. Nakushauri mpeleke Mirembe kuna mabingwa wazuri wa afya ya akili.
 
Asanteni Ndugu zangu wana Gf wote kw ushauri wenu mzuri nimepata mwanga tutafanyia kazi .Naombeni sala zenu kwa kadri ya Imani zenu.Mungua awabariki.
 
Kifafa mkuu hiyo ilimtokeaga dadaake na rafiki yangu na alipona kwa tiba za jadi japo amefariki kwa ugonjwa mwingine kabisa,alikuwa anang'ata na kutafuna hadi mchanga
cc. Mzizi mkavu mshana jr
Yah hicho ni kifafa.
Hospitali hakuna tiba zaidi ya vipimo viiiiiingi na hela ndefu.

Tiba ya uhakika ni kienyeji aka tiba asili.

Maombi kwa wenye imani angalau kama punje ya haradali.
 
Unampa Habari za Yesu, ila unataka aje sirini! we ni mpuuzi sana, unataka umtapeli?
Mbona habari za Yesu wengine wanazitangaza kwa vipaaza sauti ili kila mtu asikie?
Mkuu kumfuata mtu PM sio kumtapeli, pia sio habari za YESU tu hata habari za waganga zinatangazwa kwenye vipaza sauti.

Nilitaka kumpa mawasiliano yangu ya simu lakini sikupenda kuyaweka hadharani.

Labda nilikosea namna ya kuwasilisha ila kwa masuala ya kanisa hakuna kuombana kiingilio wala gharama yoyote.

Bado nasisitiza aje kwa YESU anaokoa kama anaamini anitafute nimpeleke kwa mchungaji ninapoabudia nataraji atapona kwa sababu wapo wengi waliokuja na matatizo kama yake na wapo huru.

Ahsante.
 
Je, akianguka anatokwa na haja ndogo?, je kwenye ukoo au familia yenu uliwahi kusikia kama hali kama hiyo ilishawahi kumtokea mtu huko nyuma?
Jinsi ulivyoeleza inawezekana baba yako ana dalili za msingi za ugonjwa wa kifafa. Ila endeleeni kutafuta uhakika hospitali kubwa
 
Pole sana. Mzee wako anatatizo la mishipa midogomidogo inayopeleka damu kwenye ubongo. Ilishapasuka ndio maana huwa anaanguka. Mpeleke Tumaini hospital.kamuone Dr. Komba au Mhimbili huwa anapart hizo sehemu mbili.
 
Mwambie ale mafuta ya nazi vijiko kumi kwa siku.. Aweke kwenye chakula ama uji.. Pia anaweza akatafuna nusu nazi kwa siku.
 
Nina ndugu yangu alikuaga anatatizo Kama hilo hivyo hivyo ulivyolezea..alizunguka kila hospital na kufanya vipomo vingi Sana baadae akagundulika Ana tatizo na nerves kichwani akapewa dawa za kutumia kwa muda was miaka miwili na kila baada ya miezi 3 anaenda kufanya vipomo miaka miwili inaisha february mwakani na hajawahi kuanguka tena..tuwasiliane labda naweza nikakusaidia hata kwa kukuelekeza ukamuone nani
 
usije ukaenda kwa waganga was kienyeji..tulizunguka kwa waganga wote wa Tanzania Hilo sio tatizo la huko..ni nerves kichwani ndo tatizo..maelezo yako na ya ndugu yangu ndii hivyo hivyo
 
Kuna jamaa yangu mama yake mdogo alikuwa na tatizo kama hilo kalazwa Muhimbili muda pamoja matibabu mengi bado hukupona haraka.
Jamaa zake wakamshauri ampeleke kwenye maombi sasa hivi majuzi namuulizia vipi mgonjwa hali yake ikoje kwa ssa? akanijibu "usicheze na Yesu" baadaye ndo akanipa mkanda mzima kuwa aliombewa akatapika sana mpaka sasa nimzima kabisa!!
Nilitaka kujua ilivyokuwa kwasababu hali ya mgonjwa nilikuwa naifahamu sema tu jamaa alikuwa na haraka ya safari. Baadaye ndo nikampigia simu akanipa mkanda habari ndefu kuhusu maombi.
Alinitajia jina la Mchungaji aliyemuombea kwamba anaitwa PARAPANDA na kwamba yuko Dar es salaam Tanzania . Japokuwa jina lake linatisha ila kwa vile muhusika anadhibitisha mama yake alipona haina shida.Nakushauri nenda Hospitali lakini pia
Mtafte huyu mchungaji
U.T.A.P.E.L.I.
 
Nina ndugu yangu alikuaga anatatizo Kama hilo hivyo hivyo ulivyolezea..alizunguka kila hospital na kufanya vipomo vingi Sana baadae akagundulika Ana tatizo na nerves kichwani akapewa dawa za kutumia kwa muda was miaka miwili na kila baada ya miezi 3 anaenda kufanya vipomo miaka miwili inaisha february mwakani na hajawahi kuanguka tena..tuwasiliane labda naweza nikakusaidia hata kwa kukuelekeza ukamuone nani
Sema hapahapa ili iwe kwa msanufaa ya wengi
 
Back
Top Bottom