Msaada: Baba yangu ana tatizo la kuanguka na kukakamaa mwili huku akisaga meno

Msaada: Baba yangu ana tatizo la kuanguka na kukakamaa mwili huku akisaga meno

Nakumbuka kuna mwalimu wangu secondary alikuwa na tatizo hili la kifafa...inashauriwa mtu huyo akienda sehemu asiwe peke yake pia asiwe karibu na moto au jiko, sisi tulikuwa tunamsindikìza mwalimu nyumbani
 
Mpeleke kanisani atapona kwa Gwajima namimi yalinitokea kama baba yako but now amepona kabisa
 
Kama kichwa cha habari hapo juu kinavyo jieleza wapendwa wangu wana JF wenzangu :

Baba yangu ni mgonjwa yapata miaka mitatu,matibabu amepatiwa bila mafanikio,na anatibiwa kwa kubahatisha kwani ugonjwa haujalikani.

Ugonjwa wake ni kuanguka na kukakamaa mwili huku akisaga meno,tatizo hili humtokea baada ya mwezi au miezi miwili.

Naombeni msaada wenu wa mawazo,ushauri kujua ni tatizo gani au kama kuna mtu alisha wahi uguza mgonjwa wa hivi.

Ni zaidi ya maumivu kwangu kumwona Baba vile nisaidieni Ndugu zangu asanteni.
Hilo ni tatizo la kifafa
Mpeleke kwa Baba Gody mwanza akaombewe
Mama yangu alishampeleka mtu aliyekuwa na tatizo ka hilo akaombewa na sasa ni mzima
Kama hospitali wameshindwa huna jinsi
 
Hopefully ni kifafa kuna dawa za miti shamba ikiwa bado haja ungua moto kuna posibility anaweza kupona.Mpeleke kwa waganga wa jadi.
 
Je, akianguka anatokwa na haja ndogo?, je kwenye ukoo au familia yenu uliwahi kusikia kama hali kama hiyo ilishawahi kumtokea mtu huko nyuma?
Jinsi ulivyoeleza inawezekana baba yako ana dalili za msingi za ugonjwa wa kifafa. Ila endeleeni kutafuta uhakika hospitali kubwa
Kwenye ukoo Hanna,hotokwi na haja ndogo
 
usije ukaenda kwa waganga was kienyeji..tulizunguka kwa waganga wote wa Tanzania Hilo sio tatizo la huko..ni nerves kichwani ndo tatizo..maelezo yako na ya ndugu yangu ndii hivyo hivyo
Wa kwako alipona Mkuu,alitumia nini?
 
Naomba kuongezea nyama kidogo,Kabla ya kupoteza fahamu huwa anapatwa na kichefuchefu kikali anapiga kelele mwisho anaanguka na kusaga meno
 
Kwenye ukoo Hanna,hotokwi na haja ndogo

Mkuu poleni sana, naomba tu muendelee kucheki hospitali kubwa hizo zinazosemwa hasa kama mna bima. Kama hamna bima mnaweza kujiunga na ile bima cjui inaitwa HIF. Lakini pia endeleeni kutafuta hata dawa sa kiasili (kienyeji) sijasema muende kwa wanganga wa kienyeji bali mtafute dawa za asili maana magonjwa kama hayo yalikuwepo na jamii zilikuwa na namna ya kuyatibu hata kabla ya uwepo wa hospitali.
 
Ikonda walipomchunguza kichwani kw x-ray hawakuona chochote zaidi walitoa dawa kuahidi wanapeleka picha India kwa uchunguzi zaidi
mkuu ikonda pale saizi ni jina tu, ni pa kawaida sana japo wanajali sana wagonjwa, pia x ray haitoshi kabisa hapo....., CT scan ya ubongo ingefaa zaidi, na inapatikana hospital chache kama ulivyoshauriwa hapo juu. pole sana,
 
Hilo ni tatizo la kifafa
Mpeleke kwa Baba Gody mwanza akaombewe
Mama yangu alishampeleka mtu aliyekuwa na tatizo ka hilo akaombewa na sasa ni mzima
Kama hospitali wameshindwa huna jinsi
Bado huyu mtu yupo mbooona nasikia.....wafuasi wake wanasema atarudi tena kama Yesu?
 
Kama kichwa cha habari hapo juu kinavyo jieleza wapendwa wangu wana JF wenzangu :

Baba yangu ni mgonjwa yapata miaka mitatu,matibabu amepatiwa bila mafanikio,na anatibiwa kwa kubahatisha kwani ugonjwa haujalikani.

Ugonjwa wake ni kuanguka na kukakamaa mwili huku akisaga meno,tatizo hili humtokea baada ya mwezi au miezi miwili.

Naombeni msaada wenu wa mawazo,ushauri kujua ni tatizo gani au kama kuna mtu alisha wahi uguza mgonjwa wa hivi.

Ni zaidi ya maumivu kwangu kumwona Baba vile nisaidieni Ndugu zangu asanteni.

Hizo zinaitwa convulsions.

Inawezekana ana uvimbe kichwani au shida nyingine kwenye ubongo.

Fanya hivi. Mtafutie mzee bima NHIF kisha fanya namna ufike Muhimbili.
Unaweza ukaomba rufaa hapo hospitali ya mkoa wenu.

Kwa muhimbili atapata vipimo vinavyostahiki CT scan au MRI na kwa kuwa utakuwa una bima, itakusaidia gharama.

Usipoteze muda kwa waganga wa jadi na mitishamba.
 
Back
Top Bottom