Msaada; Biashara ya kusafirisha abiria

Msaada; Biashara ya kusafirisha abiria

Kama bado hujanunua hiyo gari nakushauri nunua Fuso (Tipper) iwe inabeba mchanga Kibaha inaleta Dar Mbezi hesabu kwa siku laki had laki na 20, inalipa sana ukipata dereva mzuri au ukiwa unaendesha mwenyewe inaweza ikakaa had miaka 6 bado mbichi
Habari wakuu,
Nina wazo la kufanya biashara ya kusafirisha abiria kwa kutumia basi ndogo aina ya Costa ambayo nategema kufanyia mkoani lakini bado nafanya utafiti nijue ni route ipi nzuri hasa itakayo kua na Barabara ya lami

Naomba kujua mambo yafuatayo kutoka kwa wazoefu wa hii biashara

1.Bei ya Costa hasa(Nissan Civilian) ni kiasi gani kwa kununua hapa nchi au kuagiza na inakua imetembea kama ngapi?
2.Costa hii ina uwezo wa kubeba wastani wa watu wangapi(level seat)? Na vipi kuhusu uimara wake

3.Gharama za kulipia bima na usajili kwa ajili ya kutumia kwa biashara ni kiasi gani

4.Kwa route ya kwenda km 100 naweza kuingiza kiasi gani kama itaenda Mara 2 kwa siku ukitoa gharama za mafuta nk

5.Pia kwa hapa Dar Costa ya namna hio inalaza sh.ngapi kwa siku?

6.Chochote ninachohitaji kujua kuhusu biashara hii ikiwemo changamoto zake kwani sijawahi kabisa kuifanya

N:B
Safari ya km 100+makadirio ya nauli ni sh. 5000

Karibuni kwa msaada wa mawazo

View attachment 1079420
 
Kama bado ujanunua hyo gari nakushauri nunua Fuso (Tipper) iwe inabeba mchanga kibaha inaleta dar mbezi hesabu kwa siku laki had laki na 20, inalipa sana ukipata dereva mzuri au ukiwa unaendesha mwenyewe inaweza ikakaa had miaka 6 bado mbichi
Bei ya Tipper ni kiasi gani?
 
Boss wangu aliagiza sikumbuki alinunua bei gan kule ila had vibari kufunga taili mpya kupeleka bodi had tunaanza kazi anasema ilimtoka kama M80
Du poa mkuu huko sina uwezo napo
 
Mkuu nashukuru kwa kuchangia na kuja na wazo mbadala lakini nina maswali kadhaa

1.Nini changamoto za biashara niliyoweka hapo juu ili hata nikiamua kuachana nayo kama ulivyoshauri niwe nimepata majibu ya kile nilichouliza na hizo changamoto hakuna namna ya kukabiliana nazo?

2.Ni kweli biashara inaweza isiwe mpya lakini bado uhitaji wake ukawa mkubwa hasa maeneo ya vijijini huduma kama afya na usafiri bado tuachane nazo?

3.Umesema huduma ya kukusanya takataka lakini kumbuka huduma hii ipo mjini tu,huko vijijini hakuna hii huduma maana watu huchimba mashimo na kuzichoma,huku mjini pia inahitaji mtaji mkubwa kwa ajili ya vifaa vya kazi tofaut na mtaji mdogo tofauti na mtaji nilionao Mimi?

Mwisho nakushukuru kwa mchango wako wa mawazo mbadala ingawa pia hujaweka mchanganuo na changamoto ya kila mojawapo maana siamini kama kuna biashara isiyo na changamoto kabisa
Mkuu zingatia sana hiki kilichosemwa hapa.
Yaani jamaa Ana akili nyingi Kama zangu.
Mimi mwenyewe huwa nahofia sana kuingiza pesa kwenye biashara hizi common ambazo kila mtu anazifanya.
Huwa napenda ideas mpya Kama hizi hata watu wakija kuziiga unakuta ushatajirika tayar.
Hata wachina wanaokuja huku huwa wanatoboa kwa staili hyo.
 
Nimezingatia na ndio maana nikamuuliza maswali ya muhimu hapo juu,maana hata vitu vipya pia vina changamoto ambazo baadhi unaweza kuzijua lakini zingine unaweza usizijue kutokana na upya wake
Nashukuru kwa mchango pia
 
Siri ya mafanikio kwenye biashara ya usafirishaji ni jinsi ya kumpata dereva mwaminifu.
Ukimpata dereva mwaminifu faida ipo.
 
Ungeomba ushauri KABLA hujanunua hiyo gari, Mimi ningekushauri uachane na hiyo biashara na uwekeze kwenye kilimo!
Biashara ni kukabili changamoto, hicho kilimo unachodhan ni salama kuna rafiki yangu mmoja kapata hasara ya mbolea peke yake mil17 mwaka huu tu, baki mbegu, manpower maandalizi na maandalizi ya shamba,
 
Ni kweli mkuu changamoto kila mahali,hakuna biashara isiyo na changamoto,cha muhimu ni kujua mbinu za kuzikabili
 
Nissani civilian toka japan ni kuanzia 38M

Coaster mayai kuanzia 45M

Coaster box ( with 14B engine) kuanzia 55M.

Rosa kuanzia 30M
Hizi ni gharama za kila kitu hadi kuisajili kwa biashara?
 
Biashara ni kukabili changamoto, hicho kilimo unachodhan ni salama kuna rafiki yangu mmoja kapata hasara ya mbolea peke yake mil17 mwaka huu tu, baki mbegu, manpower maandalizi na maandalizi ya shamba,
Mpe pole rafikiyo! Nimeongea kutokana na uzoeafu ktk biashara zote hizo! Mimi baada ya kufanya biashara ya usafirishaji ikaniangusha! Lakini kilimo kikaniinua! Hiyo nimemshauri kama alivyo omba sijamlazimisha! Na kilimo nilicho ongelea NI cha kitaalamu sio hiki cha kutegemea mvua!
 
Biashara yoyote inayohusisha chombo Cha moto mtaji wa kwanza kabisa ni kuwa wewe mwenyewe uyajue hayo magari, yaan mechanically uwe at least una idea nayo
Kama Huna idea kabisa jitahidi msimamizi wako awe nayo,, ukiingia kwenye biashara hiyo huku Huna abcd zake utakuja juta Sana, fundi tu anaweza akakuingiza chaka na ukapotea kabisa, bado dereva na kondakta wake, bado trafiki n. K

Mtoa Mada nilivokusoma tu bado unatakiwa uyajue vizuri hayo magari or else utapotea kwa hasara, kukupa mwanga tu daladala mitumba kuna Aina kama tatu ninazozijua
1 Toyota coaster hii nzuri na imara ila ghali
2 Nissan civilian hii ni cheap ila spea ghali na manunuzi ni poa
3 Mitsubishi Rosa, hii iliwahi kudharaulika Sana mwanzoni lakini ni imara tu na haina bei kali ya manunuzi

Unpoanza biashara ya Gari jaribu kuwa na tools za bei chee ili ikue haraka na kutawanya risks, mathalan badala ya kununua Costa la mil 70 kwa nini usinunue Rosa 2 bei hiyo hiyo?
 
Part 2
Ili uweze kufanikiwa kwenye biashara ya usafirishaji unatakiwa kuwa na mambo yafuatayo

1. Uwe n gerage ya kwako hata kama ni ndogo

2. Uwe na duka la spare la kwako

3. Uwe unajua kutunza fedha zinazo kusnywa.
Habari wakuu,
Nina wazo la kufanya biashara ya kusafirisha abiria kwa kutumia basi ndogo aina ya Costa ambayo nategema kufanyia mkoani lakini bado nafanya utafiti nijue ni route ipi nzuri hasa itakayo kua na Barabara ya lami

Naomba kujua mambo yafuatayo kutoka kwa wazoefu wa hii biashara

1.Bei ya Costa hasa(Nissan Civilian)ni kiasi gani kwa kununua hapa nchi au kuagiza na inakua imetembea km ngapi?
2.Costa hii ina uwezo wa kubeba wastani wa watu wangapi(level seat)?na vp kuhusu uimara wake

3.Gharama za kulipia bima na usajili kwa ajili ya kutumia kwa biashara ni kiasi gani

4.Kwa route ya kwenda km 100 naweza kuingiza kiasi gani kama itaenda Mara 2 kwa siku ukitoa gharama za mafuta nk

5.Pia kwa hapa Dar Costa ya namna hio inalaza sh.ngapi kwa siku?

6.Chochote ninachohitaji kujua kuhusu biashara hii ikiwemo changamoto zake kwani sijawahi kabisa kuifanya

N:B
Safari ya km 100+makadirio ya nauli ni sh. 5000

Karibuni kwa msaada wa mawazo

View attachment 1079420
 
Biashara yoyote inayohusisha chombo Cha moto mtaji wa kwanza kabisa ni kuwa wewe mwenyewe uyajue hayo magari, yaan mechanically uwe at least una idea nayo
Kama Huna idea kabisa jitahidi msimamizi wako awe nayo,, ukiingia kwenye biashara hiyo huku Huna abcd zake utakuja juta Sana, fundi tu anaweza akakuingiza chaka na ukapotea kabisa, bado dereva na kondakta wake, bado trafiki n. K

Mtoa Mada nilivokusoma tu bado unatakiwa uyajue vizuri hayo magari or else utapotea kwa hasara, kukupa mwanga tu daladala mitumba kuna Aina kama tatu ninazozijua
1 Toyota coaster hii nzuri na imara ila ghali
2 Nissan civilian hii ni cheap ila spea ghali na manunuzi ni poa
3 Mitsubishi Rosa, hii iliwahi kudharaulika Sana mwanzoni lakini ni imara tu na haina bei kali ya manunuzi

Unpoanza biashara ya Gari jaribu kuwa na tools za bei chee ili ikue haraka na kutawanya risks, mathalan badala ya kununua Costa la mil 70 kwa nini usinunue Rosa 2 bei hiyo hiyo?
Nimekupata mkuu,lengo hasa ni gari moja tu kama ni Nissan Civilian kwakua sijawa na uwezo wa zaidi ya hapo maana bajeti niliopigia kichwani ni 30M so sijajua maana hapo juu hujaweka makadirio ya bei kwa kila moja lakini nashukuru nimepata mawazo yako
 
Back
Top Bottom