MSAADA: Biashara zinanivuruga naona nachanganyikiwa. Nifanyeje kujitoa katika hali hii?

MSAADA: Biashara zinanivuruga naona nachanganyikiwa. Nifanyeje kujitoa katika hali hii?

Kama ambavyo mgonjwa asipopima kwa kipimo sahihi, hatopata dozi sahihi na hatimaye hatopona.

Binafsi sijaelewa nini changamoto unayopambana kuitatua? Kama mitaji kibongo bongo uko mbali ,

1.Je ulipanga mauzo kwa mwaka kila biashara yafike kiasi gani na umefikia /feli kwa % ngapi?

2.Je una wateja wengi kuliko mtaji unataka mkopo au partner?

3.Location mbovu, je utamudu location unayoona nzuri na ikatokea mauzo yakabaki kama yalivyo sasa?

Weka wazi eneo lipi linalokunyima usingizi
 
Hapo ndo unapokosea.. watu hutoka huko kwenye makazi na kwenda kununua godoro kariakoo. Ukiwapelekea iyo huduma huko unakoita kwenye makazi huoni ni rahisi kuwapata? Hivyo hivyo kwa hizo electronics?
Ww wabongo huwajui….
Mtu anaruka maduka ishirin y magodoro mtaani kwake anaenda nunua kariakoo
 
Mm siwez mshauri mtu mwenye maduka 5, ni matumizi mabaya ya akili na elimu yng kwny business…

Labda kama n maduka y urithi, bt haiingii akilini ufungue duka la kwanza mtaji 8 million, duka la pili 7 million, duka la 3, la 4 mpaka la tano zen ucjui kutatua changamoto za biashara zako? Non sense…

Labda uwatafute washauri wa maswala ya biashara, hopefull ada zao unazimudu maaana details zenyewe za biashara zako hujaziweka wazi…

Maduka matano picha moja… hahaha Bongo shkamooo 🙌🏽
 
Hapo ndo unapokosea.. watu hutoka huko kwenye makazi na kwenda kununua godoro kariakoo. Ukiwapelekea iyo huduma huko unakoita kwenye makazi huoni ni rahisi kuwapata? Hivyo hivyo kwa hizo electronics?
...kuna baadhi ya wateja hatakama bidhaa inapatikana mtaani kwake, yuko radhi kwenda kariakoo. Yani hua na kaimani flaani kua huko kuna unafuu flani interms of cost minimization(reasonable cost), Quality,quantity, pia uwanja mpana wa kuchagua(freedom of choice) tofauti na akija dukani kwako
 
Mchele upo location gani? Nikutajie sehem ambazonunaweza weka mchele ukatoboa kirahis maana ndo bizzness yang hiyo
Kaka Mimi nipo dar es salaam nahitaji anzisha hiyo biashara naomba location nzuri
 
Habari ndugu, naomba niwashirikishe kidogo yanayonisibu;

Nina biashara 5;
1. Magodoro
2. Electronics
3. Mchele
4. Duka la rejareja
5. Vinywaji vya jumla.

Kinacho niumiza wakuu chakwanza ni location mbovu haswa kwa biashara ya;
1. Mchele
2. Electronics
3. Magodoro

Jambo la pili ni mtaji hautoshelezi vizuri kutokana na kufeli kupata hela nilizotarajia kujazia zaidi mchele na vinywaji vya jumla na matibabu ya mdogo wangu yamenikwangua fedha.

Nashindwa kuamua niue biashara gani kuimarisha nyingine na zote nazipenda zaidi, nafeli location zaidi
kwani mitaji zimebeba sio mbaya mfano electronic imebeba about 8M, Magodoro about 7M, Mchele nina tani 4.

Naombeni msaada najitoa vipi kwenye hii hali. Sehemu inayohitaji mtaji zaidi ni vinywaji vya jumla haswa na kuna onesha mafanikio kukipewa mtaji.

Nifanyeje kujitoa kwenye hii hali. Siwezi kupata mkopo sijaajiriwa na sina nyumba.

Pia soma: Nina mtaji wa milioni 10 nifanye biashara gani
Kwa Nini usibaki na biashara moja au mbili unazofanya vizuri ukawa na location nzuri na usimamizi mzuri. Biashara kuwa nazo nyingi tofauti tofauti wkt management yake Bado pia inakupasua kichwa utajikuta mtaji unavuja sehemu.
 
Unaweza kupata mkopo ASA wanatoa mkopo kwa wanaume pia sio kwa vikunei vya kina mama pekee.
Hata microfinance kama ile zamani ilikuwa inaitwa Access sasahivi imebadilishwa jina inaitwa
 
Back
Top Bottom