Ngoja nikuambie namna nilijifunza kupika wali,
chemsha maji kiasi yachemke vyema, kisha tia chumvi, (utajua kwanini tunatia chumvi)..
kisha tia mchele wako ambao umeshauandaa vyema, baada ya hapo sasa punguza maji, hakikisha maji na mchele havipishani sana wingi, (hili zoezi liwe la haraka ili mchele usishike chini), kumbuka hapo mafuta hatujatia bado..
ndiposa uweke mafuta, jitahidi mafuta yako yawe kwenye chombo kidogo, usipende kutumia kidumu moja kwa moja, ni rahisi kumimina mengi..!!
as I told you Jana, funika wali wako, ukishachemka vyema, punguza moto hadi mwisho kabisa, maji yakikaukia ukaona wali wako bado mgumu ndipo tunaongeza yale maji moto yenye chumvi tuliyopunguza mwanzoni, usitie maji baridi wala usitie maji yaso chumvi, chakula chako kitapoteza ladha kabisa..!!
ukishazoea sasa vipimo vya maji, chumvi na mafuta ndiyo unaruhusiwa kupika kwa mbwembwe as you can..!!