Msaada/confession: Sijui kupika wakuu

Msaada/confession: Sijui kupika wakuu

Wenzako wanajifunzia kupika kwenye mapupu, wanaenda machinjioni wanachukua kende za ng'ombe na kwenda kujifunzia kupika kama kutengeneza supu na kuunga mboga

Kende za ng'ombe tena? 😂😂
 
Ngoja nikuambie namna nilijifunza kupika wali,

chemsha maji kiasi yachemke vyema, kisha tia chumvi, (utajua kwanini tunatia chumvi)..

kisha tia mchele wako ambao umeshauandaa vyema, baada ya hapo sasa punguza maji, hakikisha maji na mchele havipishani sana wingi, (hili zoezi liwe la haraka ili mchele usishike chini), kumbuka hapo mafuta hatujatia bado..

ndiposa uweke mafuta, jitahidi mafuta yako yawe kwenye chombo kidogo, usipende kutumia kidumu moja kwa moja, ni rahisi kumimina mengi..!!

as I told you Jana, funika wali wako, ukishachemka vyema, punguza moto hadi mwisho kabisa, maji yakikaukia ukaona wali wako bado mgumu ndipo tunaongeza yale maji moto yenye chumvi tuliyopunguza mwanzoni, usitie maji baridi wala usitie maji yaso chumvi, chakula chako kitapoteza ladha kabisa..!!

ukishazoea sasa vipimo vya maji, chumvi na mafuta ndiyo unaruhusiwa kupika kwa mbwembwe as you can..!!

Leo usiku huu napika tena wali 😀
 
Mara nyingi vipimo ..mafuta,chumvi,maji
Mfano chapati huwa sielewi shida ni nini aise
Chapat Zina changamoto sabbu ya process nyingi ila vingine vipimo jitahid sana kwenye makadirio ukiweza kucheza na hapo chochote unapika vizuri
 
Namshukuru mama yangu tangu miaka ya 199... alinifundisha kupika hadi leo nimeiva

Ugali ulikua unatestiwa ukutani kama umeiva 😃😃😃 ukirusha ukaganda ujue umeumia
 
Back
Top Bottom