Msaada/confession: Sijui kupika wakuu

Msaada/confession: Sijui kupika wakuu

Wakuu,

Nilishawahi kuleta uzi wa kutojua kupika way back Mwanamke kutojua kupika inaweza kuwa sababu ya kupewa talaka?
Jioni hii nimepika wali...nauangalia hapa naona aibu mimi...wali una mafuta huoo

Nilianza kujua kupika lakini sjui nimesahau ama ni vipi lakini kila nikipika naharibu 🙌

Nisaidieni tips za kujua kupika vizuri...

Aaliyyah
Mwachiluwi
Sis Carleen

Bro Evelyn Salt nisaidie braza
Ebo! Kumbe Evelyn Salt ni ana makende 😲😲😲
Sasa wee ujue kupika ili iwaje? Hizo mechi za o2.5 sii zinakupa hela ya kuweza kuoda chakula. Muhimu kula...mume akitaka chakula unampeleka serena ale mpaka achoke
 
Nenda chuo cha mapishi ndani ya mwezi tu. Unakuwa profeshional
 
Wanawake asilimia kubwa Ku pika huwa hawajui Ila wanachojua ni kujipikilisha.

Unakuta mtu anapika wali na dagaa masaa kibao mara aweke maji ananyunyuzia hatari tupu.


So haupo peke yako .

Jaribu kujifunza youtube wanaume wanavyopika kuanzia kuandaa vyombo hadi kupika
 
Mbona mie wali naupika kwa mfumo huo uliowashangaza wa maji ya baridi 😀

Nitajitahidi kupika mara nyingi nikiweza, asante sis 🙏
Ngoja nikuambie namna nilijifunza kupika wali,

chemsha maji kiasi yachemke vyema, kisha tia chumvi, (utajua kwanini tunatia chumvi)..

kisha tia mchele wako ambao umeshauandaa vyema, baada ya hapo sasa punguza maji, hakikisha maji na mchele havipishani sana wingi, (hili zoezi liwe la haraka ili mchele usishike chini), kumbuka hapo mafuta hatujatia bado..

ndiposa uweke mafuta, jitahidi mafuta yako yawe kwenye chombo kidogo, usipende kutumia kidumu moja kwa moja, ni rahisi kumimina mengi..!!

as I told you Jana, funika wali wako, ukishachemka vyema, punguza moto hadi mwisho kabisa, maji yakikaukia ukaona wali wako bado mgumu ndipo tunaongeza yale maji moto yenye chumvi tuliyopunguza mwanzoni, usitie maji baridi wala usitie maji yaso chumvi, chakula chako kitapoteza ladha kabisa..!!

ukishazoea sasa vipimo vya maji, chumvi na mafuta ndiyo unaruhusiwa kupika kwa mbwembwe as you can..!!
 
Pendelea kupika Kila wakat pindi unapopika Kila mara ndipo unapoweza jua wap unakosea kesho Tena unarekebisha then unakaa sawa
 
Itabidi utafute mwanamume anaejua kupika kama Mwachiluwi ili mgawane majukumu mkuu 😅😅😅... Jokes.

All in all kupika ni sanaa so sio kila mtu anaweza kuimudu hiyo sanaa, kuchanganya changanya mavitu vitu hadi itokee kitu yenye ladha moja sio mchezo😅😅
Yes, cooking is art.
Some times you need to practice alot in order to achieve perfection.
Like every other arts, some people need one time and others need few more times to succeed.
Joanah aendelee hivyo hivyo kujaribu atafanikiwa au hatafikia kiwango cha wengine na siyo lazima afikie hakuna kujisikia vibaya. Yeye lazima atakuwa bora kwenye sanaa zingine.
 
Nakumbuka kazini tulichangisha donei nikasema niacheni niisimamie show nilipika dagaa waliokaangwa kwenda kwenye mchuzi nikaweka na kindimu kwambaali aisee mademu tulikua tunafanya nao kazi walinipa bigup wakawa wananiambia au ulisomea hotel management 🤣🤣🤣🤣
 
Yes, cooking is art.
Some times you need to practice alot in order to achieve perfection.
Like every other arts, some people need one time and others need few more times to succeed.
Joanah aendelee hivyo hivyo kujaribu atafanikiwa au hatafikia kiwango cha wengine na siyo lazima afikie hakuna kujisikia vibaya. Yeye lazima atakuwa bora kwenye sanaa zingine.
Umenena vyema mkuu.
 
Joanah mbona kupika sio kitu chenye ugumu hivyo!
Labda mtindo wa makuzi yako ulikuweka mbali na mapishi lakini ni kitu rahisi sana .
Kama umepika wali umeona kuna makosa fulani kesho pika tena ukirekebisha pale ulipo kosea leo na kurudia hivyo hivyo jadi ujenge mazoea.
Hamia chakula kingine , mwisho wa siku utajikuta mpishi mzuri kuliko wengi walio na taaluma hio.

Kupika sio kitu kigumu lakini ni kigumu TBH
 
Nimelia sana! Hivi Joanah una nini?

😂😂😂😂

Kujua kupika kuna mawili, kupenda na kupata right motivation. Mfano mi sipendi at all lakini akiwepo shemeji yako nakuwa motivated kupika, So natoa kitu hatari.

Lakini amini nakwambia mapishi sio universal language, kama si chef by profession then unatakiwa kujua kupika kwa ajili ya your people if they like it then you are good. It’s okay watu ambao sio wako kusema chakula chako kibaya.

Mimi nimeshaona sipendi kupika wallah vile 😂
 
Back
Top Bottom