Msaada: Dawa ya fangasi

Atalanta

Member
Joined
May 25, 2022
Posts
72
Reaction score
251
Habari zenu wakuu natumaini mu wazima. Moja kwamoja kwenye mada...

Wakuu mimi ni kijana jinsia "me" nasumbuliwa na tatizo la FANGUS kwa muda mrefu. Nimetumia dawa mbalimbali za kunywa "fluconazol" yawezekana nimekosea kuandika Ila jina lake linaendana na hilo, pia nimetumia dawa za kupaka lakini tatizo bado halijaisha. kwa wale waliokaa hosteli wanaita "pumbu jero" Yaani fangusi wapo kwenye mapumb. Mwanzoni walikuwa wanawasha Sasa nnavojikuna ngozi inakwanguka lakini saizi hawawashi Sana Kama mwanzo Ila ngozi ya kwenye korodani inabanduka Yaani inaonekana kabisa hii ni fangus. Hospitalini nimeenda kila Mara lakini tatizo naona bado haliishi.

Kama na wewe ulishawahi pata huu ungonjwa na ukapona Basi ulitumia dawa gani..??, au Kama unaifahamu dawa yake naomba share mahali hapa kwani naamini itawasaidia na wengine wengi.

Ahsanteni
 
Safisha vizuri sehemu alafu kausha kwa kitambaa safi kisha paka asali, ndani ya wiki njoo unishukuru, zilinitesa zaidi ya miaka kumi na ushee nimepona juzi tu nasikia hata mapunye asali ni dawa
 
Safisha vizuri sehemu alafu kausha kwa kitambaa safi kisha paka asali, ndani ya wiki njoo unishukuru, zilinitesa zaidi ya miaka kumi na ushee nimepona juzi tu nasikia hata mapunye asali ni dawa
Asali ipi mkuu, mbichi??
 
Usafi wa hilo eneo ni dawa namba moja, ukavu baada ya kusafisha vizuri dawa namba mbili, fua boxer zako zitakate na anika juani/ piga pasi.. dawa namba tatu, angalizo hizo ulizonazo zote choma moto yaani achana nazo zimejaa maambukizi unakunywa dawa ila ugonjwa umeutunza kwenye boxer chafu. Baada ya hapo tumia sasa dawa ulizopewa hospital mambo ya asali sina uhakika ingawa kwa elimu yangu ya ngumbaru sidhani kama itakusaidia.
 
Tumia dawa inaitwa intraconizole

Au kama upo morogoro nikupee no ya dokta
 
Kuna ile dawa iko kama spirit ila niya kijani .una paka baada ya kuoga ila kuwasha kwake ni zaidi ya kuweka chumvi plus spirit kwenye kidonda ni kaliiiii
 
Tumia maji ya baridi kabisa kuosha pumbu, ukiweza yaweke kwenye freezer yawe ya baridi sana halafu ndo utumie kusafisha pumbu. Fanya hivyo hata mara 10 kwa siku ikiwezekana, yani hizo sehemu zipate ubaridi muda wote.

Ndani ya wiki mbili utakuwa umepona mkuu.
 
Kuna ile dawa iko kama spirit ila niya kijani .una paka baada ya kuoga ila kuwasha kwake ni zaidi ya kuweka chumvi plus spirit kwenye kidonda ni kaliiiii
Duh unamwambia apake huko? Mimi nilikuwa nimefanya kama 'ringworm' kwenye mkono nikaweka hiyo dawa bila ya kusoma maelekezo. Nilichukuwa pamba nikaweka dawa kwenye eneo lilioathirika halafu nikasugulia vizuri kwa pamba, loh! niliruka ruka kama nacheza ngoma ya kimasai. Lakini nashukuru niliweka mara mbili tu likapotea kabisa.
 
Yeye akipaka uko sijui atakua kwenye hali gani ila kwakua inasaidia apambane tu
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…