Msaada dawa ya kuvuta wateja

Yawezekana unauza bidhaa zako sehemu isiyo sahihi. Unaweza kuuza bidhaa sahihi kwa watu wasio sahihi, angalia mazingira.
 
Fanya tathmini ya kina....na ukumbuke biashra zina msimu pia, je sasa hivi ni high season Kwa biashara yako?

Unaweza kudhani watu hawaji, kumbe now biashara iko low season.

Ukifanikiwa kupata dawa Naomba nishirikishe.
Hapa hakuna cha dawa wala cha nini, kama ni dawa ni chumvi halisi ya mawe inatosha, ikibidi na kuomba kwa Mungu akufanyie wepesi biashara iende vizuri, ukienda huko kungine utaliwa pesa tu, ni kama ulivyosema biashara zina msimu, kwa mfano mimi biashara yangu kuna miezi fulani haiendi vizuri, ikipita hiyo miezi mambo yanakwenda safi tu.
 
Sijakuelewa
Hakuna dawa ya kuvuta wateja (unless kama hio dawa ni mbinu ya kumpa mteja anachotaka) either kwa ulaghai, bei ndogo, good customer services, ubora kuliko majirani au kitu ambacho wewe unacho wanaouza kama wewe hawana (hata kama wao ni bora wewe ni duni unaweza kutumia marketing na promotion; yaani good salesmanship)

Zaidi ya hapo sababu kuna wateja (kama wewe) ambao wanatafuta dawa ya kuongeza wateja; unaweza kuwaambia hio dawa unayo hence utawavuta (hata kama haifanyi kazi ni vigumu kusema haijafanya huenda utawapa confidence hence kujiamini na kupata wateja au wakifeli utasema hawakufuata masharti); By the way wateja wengine wakihisi wewe mshirikina usishangae wakaingia mitini...
 
Mdomo na ulimi wako ni dawa tosha ya eidha kuwavuta au kuwafukuza wateja,ukitaka kuamini hili wewe uwe mkali kwa wateja wako uone kama watakuja,au uwe na lugha nzuri uone kama hawatakuja!!
 
Hakuna dawa kama hiyo duniani,hapa kinachoonekana,huduma kwa wateja wako ni mbaya,ama maana ya ubora wa bidhaa,ana huduma kwa mteja ama kauli zisizo ridhisha ama uendelevu wa huduma ni wa kusuasua,na iwapo sii wewe unaye wahudumia wateja wako ni ama anayewahudumia anashida ama jinsi ya kuwahudumia wateja au unminifu wa mtoa huduma katika biashara yako.Hivyo uchawi ndio huo,hakuna miujiza ya kidawa,wala kiganga.Kama bado unampango wa kutafuta mganga nitafute mimi🤪
 
Ndo maana wabongo wengi tupo kama machizi, tunarogwa sana.... Mme/mke akuroge, mchepuko akuroge, ukikaa vibaya kazini urogwe haya hata mangi hapa nae aroge mtu utakuaje timamu jamani
Mume anakuroga uwe zezeta, mchepuko wake unakuroga uachike, boss anakuroga, jirani anakuroga...muuza chips anakuroga, bodaboda anakuroga, dukani unarogwa, sokoni ndio usiseme bado watoto wakikua wakamwana wanakuroga upunguze mdomo....afu tukizibuka akili wanatushangaa
 
Mkuu ukipata na mimi unipasie
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…