Msaada dawa ya visunzua usoni

Msaada dawa ya visunzua usoni

Wataalam wa ngozi wanasemaje kuhusu Sunzua?
Tatizo hili ninakuwa kubwa,watu wengi wanasumbuka nayo.
 
Habari wapendwa, tafadhari anayejua namna ya kuondoa visunzua usoni vile vinyama vinavyoota usoni vyeusi real vinakela Sana.

Pia ningefurahi endapo ningepata chanzo chake. Shukrani kwenu.
Sivijui hivo vitu unavyovisema ila nimehisi tu vitu flani hivi. Nina dawa 2 nakupa itakayokufaa urudishe mrejesho
1. Ukipikia kuni hazijakauka vizuri huwa zinatoa majimaji yana vimapovu, basi xhukua na kidole uchue sehem vilipo
2. Pakaa colgate narudia tena colgete ile nyeupe plain sio hizi zingine kila usiku unapolala
 
Habari wapendwa, tafadhari anayejua namna ya kuondoa visunzua usoni vile vinyama vinavyoota usoni vyeusi real vinakela Sana.

Pia ningefurahi endapo ningepata chanzo chake. Shukrani kwenu.
Kwa soma soma yangu ya hapa na pale
Kuna zile sunzua moja moja tu km usoni moja au mkononi moja ambayo hizo husababishwa na aina fulani za virus ambazo tiba zake ni kuchomwa kwa penseli maalum za chemikali.

Ila kama una vinyama vidg sana halafu vingi vyenye kutapakaa mashavuni shingoni... na hasa ukiwa na uzito wa ziada... huenda ikawa ni dalili ya insulin resistance... ulaji mbaya wa vyakula vya uwanga na sukari na mafuta mabaya

Tiba yake ni kubadilisha mfumo wa maisha wa kula kwa ujumla
 
Mkuu nakupa dawa moja hivi ambayo alitumiaga kaka yangu kabisa kipindi tupo wadogo,

Alitokwa na visunzua vingi miguuni alipelekwa hospital kubwa za wilaya, ngoma ikadunda akapelekwa hadi kule Tegeta kwa masister hali ikawa vile vile.

Siku moja tumekaa home akaja rafiki yake Mama alishangaa sana kuona vile vidude vinasumbua na vimechukua muda mrefu kupona wakati dawa yake ni ya kawaida tu.

Amini hiki ninachokwambia, alisema chukueni Mavi ya kuku yaliyokauka yasage yaweunga unga... Kisha kwenye vile visunzua fanya kama unaupaka ule unga kwa kuusugua kwenye visunzua...ndani ya wiki kadhaa tuletee mrejesho.
Asee
 
Habari wapendwa, tafadhari anayejua namna ya kuondoa visunzua usoni vile vinyama vinavyoota usoni vyeusi real vinakela Sana.

Pia ningefurahi endapo ningepata chanzo chake. Shukrani kwenu.
nimefanikiwa kuviondoa ila kwa kuvichoma japo bei yake mkasi kidogo
 
Tumia pia na hii
 
Attachments

  • IMG_20241106_163041_683.jpg
    IMG_20241106_163041_683.jpg
    247.2 KB · Views: 15
Back
Top Bottom