Msaada: Dogo janja anaimbaga nini? Sijawahi kumuelewa

Msaada: Dogo janja anaimbaga nini? Sijawahi kumuelewa

and 300

JF-Expert Member
Joined
Jun 27, 2012
Posts
26,398
Reaction score
36,406
Huyu mwanamuziki nimetokea kumfahamu pale alipofunga ndoa na binti mrembo Irene Uwoya, sasa nikaanza kusikiliza nyimbo zake.

Wajuvi wa mambo mnisaidie huyu huwa anaimba muziki wa aina gani?

Na hualikwa kwenye matamasha ama concert/show na watu wanalipa viingilio? Au anafanya hisani (bure).

Natanguliza shukrani.
 
HUyu dogo nimetokea kumfahamu pale alipodai amemuoa binti mrembo Irene, sasa nikaanza kusikiliza Nyimbo zake. Wajuvi wa mambo mnisaidie huyu huwa anaimba muziki wa aina gani? na hualikwa kwenye matamasha na watu wanalipa viingilio?au anafanya hisani (BURE). Natanguliza shukrani.
Anaimba mziki ambao ni wa kukuburudisha tu siyo wa kukuelimisha wala wa kukufanya utafakari ni mziki wa kukuburudisha tu huhitaji kuelewa sana anachoimba.
Personally toka amechange kidebe, ngarenaro, na ule mwingine jina limenitoka dogo namuelewa sana...
 
Ndugu sina chuki dhidi yake, ni katika kutaka kujua wanamuziki na muziki hapa nchini Tanzania. So far nauelewa zaidi Muziki wa Diamond, Harmonize, Ally Kiba, Ben Pol ILA BADO NAJILAZIMISHA kuwaelewa JUX, VANESSA, DOGO JANJA na ROMA.
Ukiona humwelewi huna haja ya kujilazimisha yani ingekuwa shule tungesema hilo somo siyo compulsary. Huwezi kuelewa kila mwanamziki ndiyo maana wengine wanawaelewa akina nikki mbishi wengine hawawaelewi
 
Back
Top Bottom