Msaada . Eti Punyeto Inaweza Kusababisha Maumivu Makali ya Mgongo wa Chini?

Msaada . Eti Punyeto Inaweza Kusababisha Maumivu Makali ya Mgongo wa Chini?

Shimba ya Buyenze

JF-Expert Member
Joined
Dec 22, 2014
Posts
182,097
Reaction score
1,099,383
Body-Effects-of-Masturbation.jpg

Pengine hii ingefaa iwekwe kwenye jukwaa la JF Doctor lakini naamini hapa MMU ndiyo nitapata jibu la moja moja kwa sababu memba wengi wa kile chama mashuhuri cha CHAWAPUTA wapo hapa. Kwa hiyo mods naomba please msiuhamishe uzi huu kwenda JF Doctor.

Ishu iko hivi: First born (mvulana) wa kakangu mkubwa yupo kidato cha nne na anaendelea na mitihani yake kwa sasa. Cha ajabu ni kwamba anasumbuliwa sana na maumivu ya mgongo kiasi kwamba hawezi kukaa kwa muda mrefu na wakati mwingine inabidi wamletee godoro au mkeka hapo hapo kwenye ukumbi wa mitihani ili aandike huku akiwa amelala.

Babake amehangaika sehemu mbalimbali lakini madaktari hawajagundua tatizo lolote. X-rays za mgongo na vipimo vingine vinaonyesha dogo hana tatizo. Mpaka wengine wamefikia hata kusema kuwa pengine ana tatizo la kisaikolojia tu au eti karogwa.

Juzi juzi hapa daktari mmoja akatushauri tumuulize huyu dogo kama huwa anaungurumisha mapunyeto kwa angalau mara 10/wiki. Daktari anasema kwa wavulana mapunyeto yakizidi sana yanaweza kuharibu baadhi ya neva huko chini na kusababisha maumivu makali ya mgongo pamoja na matatizo mengine kama ugumba.

Swali langu ni kwamba kuna memba ye yote mwaminifu wa CHAWAPUTA hapa ambaye ameshakumbana na tatizo hili la kuumwa na mgongo wa chini kiasi cha kushindwa kukaa kabisa (kwa sababu ya mapunyeto)? Na kama yupo alifanyeje ndiyo akapona?

Angalizo: Ni kweli nilimuuliza dogo na akakiri kuwa huwa anaungurumisha mapunyeto sana japo sasa anadai kuwa amepunguza. Nilipombana akasema huko nyuma alikuwa anakwenda trip mbili hadi tano kwa siku. Ni kweli anaweza kuwa ameathirika kiasi cha kushindwa kukaa?

Tumepanga kumpeleka kwa wanasaikolojia na watu wa therapy mara tu akimaliza mitihani yake.

Asanteni!
 
Kama doctor amekushauri hvyo.uenda ikawa ni kweli.ila napatwa na mashaka hata kama ni punyeto.inakuwaje tatizo halionekani?
 
NGOSHA IKO IVI
Watu wenye msongo wa mawazo yatokanayo na sababu mbali mbali kama KUFIWA NA MZAZI, MME , MKE au MLEZI huwa katika hatari ya kupatwa na maumivu nyuma ya shingo , mgongoni n.k maumivu ya kichwa pia MADAKTARI HUSHINDWA KUTAMBUA UGONJWA HUSIKA...Mwisho mmgonjwa huhisi karogwa ndio maanaa walio wengi hufa mapema... DOGO ANASTRESS MDODOSE VIZURI ....
 
Ni kati ya athari za punyeto hasa unapokua unaifanya kama chakula.

Baadhi hupiga punyeto japo mara mbili kwa mwezi kwaajili ya kupunguza shahawa zilizojitengeneza maana hata ukiacha zitatoka ukiwa usingizini.

Hawa vijana wanaopiga punyeto kama starehe ndo hupata maradhi haya.
 
Aiseeee hali inatisha. Inawezekana ikawa kweli endapo alikuwa akiungurumisha mara nyingi. Hiyo kitu achana nayo kabisa kwani ina mzuka wake. Hadi uje uiache itakuchukua muda halafu itakutaka uwe na Ke ya uhakika home. Akimaliza tu mtafutieni Ke amalizane naye daily aachane na mgalala
 
Hiyoo kwelii aisee me mwenyewee nime8piga sana nikiwa Ndanda boys ndo maan nikijapata mwanangu siji mpeleka boarding za boys ni mchanganyikoo
Maana me ilikuwa hata kila nikioga aisee
Nimehangaika sana aisee sema Niko sawaa but mkipeleka mtafutieni na dem na msimuache mwenyewee na kama anahoby hasa ya mpira au any active activities anaweza fsnyaa
 
Aiseeee hali inatisha. Inawezekana ikawa kweli endapo alikuwa akiungurumisha mara nyingi. Hiyo kitu achana nayo kabisa kwani ina mzuka wake. Hadi uje uiache itakuchukua muda halafu itakutaka uwe na Ke ya uhakika home. Akimaliza tu mtafutieni Ke amalizane naye daily aachane na mgalala

Ndiyo ni mgalala na wengi tunaichukulia kama sehemu ya ukuaji wetu hasa kuvuka kile kipindi kigumu cha kujitambua cha balekhe. Sasa kweli mtu unapiga mgalala mpaka unachakachua mgongo na bado tu hushtuki? Huyu akija kuzeeka itakuwaje? Na si ajabu huko aliko kila akiweza anaungurumisha japo mgongo nyang'anyang'a. Ndiyo maana tunataka tujaribu watu wa saikolojia na wataalamu wa mambo ya uraibu.
 
Kama doctor amekushauri hvyo.uenda ikawa ni kweli.ila napatwa na mashaka hata kama ni punyeto.inakuwaje tatizo halionekani?
Madaktari walikuwa wanadhani kuwa pengine baadhi ya pingili za uti wa mgongo zina mushkeli ndiyo maana wametusisitiza sana tukumbuke kama alishawahi kupata ajali yo yote, kuanguka kwenye baiskeli au kujiumiza katika michezo. X-rays zote zinaonyesha uti wa mgongo uko sawa ndiyo maana wote tuko puzzled mpaka huyu Dr. wa mwisho aliyegusia ishu ya punyeto. Ngoja tuendelee kuhangaika na nitaleta mrejesho itakavyokuwa.
 
Acha upumbavv wewe.... Unaleta utoto kwa serious issues???????
Huna cha kushauri kaa kimya....

pumbavv wewe... jinga kabisa.

[HASHTAG]#Chief[/HASHTAG] Eng.
Pole pole Chief Engineer. Kuna thread nyingi za punyeto hapa na watu wanaweza kuwa wameshachoka nazo. Nimepitia karibu zote lakini sijaona inayogusia maumivu ya mgongo. Response ya huyo mdau inaeleweka.
 
Fluids zinaisha ukipiga nyeto sana ndio maana unamuona mtu akinyoosha mguu ,maeneo ya goti hutoa sauti fulani na hata kwenye mgongo na maungio mengine

Huyo dogo anafululiza nyeto sana jambo linalosabahisha fluids kuisha na hvy kupelekea maumivu kwenye mgongo pindi anapokaa sana na pia huyo hata kukimbia hatoweza sabb miguu itamuuma

Onyo:upigaji wa nyeto kupita kiasi ni hatari kwa nguvu zako
 
Asante mkuu. Kwa hiyo akinywa maji mengi kama Ray Kigosi inaweza kumsaidia? Au ni fluids za aina gani atumie?
 
Asante mkuu. Kwa hiyo akinywa maji mengi kama Ray Kigosi inaweza kumsaidia? Au ni fluids za aina gani atumie?
Shahawa inatengenezwa na vitu vingi na moja ya vitu hvy ni semen ,semen ni fluid ambayo hutengenezwa kwenye bone marrow,unavyopiga nyeto basi mfululizo basi utapoteza idadi kubwa ya semen..ni kama vile grisi kwenye baiskeli pindi inapoisha ukakamavu hutokea hvy hvy kwenye mifupa ,semen ni kama grisi vile kwenye chuma

Dawa ni kula chakula kwa wingi ili semen zizalishwe kwa wingi ..na aache nyeto kwa muda wa wki 2,3 halafu ale msosi atarudi kwenye hali yake ya kawaida
 
Back
Top Bottom