Shimba ya Buyenze
JF-Expert Member
- Dec 22, 2014
- 182,097
- 1,099,383
Pengine hii ingefaa iwekwe kwenye jukwaa la JF Doctor lakini naamini hapa MMU ndiyo nitapata jibu la moja moja kwa sababu memba wengi wa kile chama mashuhuri cha CHAWAPUTA wapo hapa. Kwa hiyo mods naomba please msiuhamishe uzi huu kwenda JF Doctor.
Ishu iko hivi: First born (mvulana) wa kakangu mkubwa yupo kidato cha nne na anaendelea na mitihani yake kwa sasa. Cha ajabu ni kwamba anasumbuliwa sana na maumivu ya mgongo kiasi kwamba hawezi kukaa kwa muda mrefu na wakati mwingine inabidi wamletee godoro au mkeka hapo hapo kwenye ukumbi wa mitihani ili aandike huku akiwa amelala.
Babake amehangaika sehemu mbalimbali lakini madaktari hawajagundua tatizo lolote. X-rays za mgongo na vipimo vingine vinaonyesha dogo hana tatizo. Mpaka wengine wamefikia hata kusema kuwa pengine ana tatizo la kisaikolojia tu au eti karogwa.
Juzi juzi hapa daktari mmoja akatushauri tumuulize huyu dogo kama huwa anaungurumisha mapunyeto kwa angalau mara 10/wiki. Daktari anasema kwa wavulana mapunyeto yakizidi sana yanaweza kuharibu baadhi ya neva huko chini na kusababisha maumivu makali ya mgongo pamoja na matatizo mengine kama ugumba.
Swali langu ni kwamba kuna memba ye yote mwaminifu wa CHAWAPUTA hapa ambaye ameshakumbana na tatizo hili la kuumwa na mgongo wa chini kiasi cha kushindwa kukaa kabisa (kwa sababu ya mapunyeto)? Na kama yupo alifanyeje ndiyo akapona?
Angalizo: Ni kweli nilimuuliza dogo na akakiri kuwa huwa anaungurumisha mapunyeto sana japo sasa anadai kuwa amepunguza. Nilipombana akasema huko nyuma alikuwa anakwenda trip mbili hadi tano kwa siku. Ni kweli anaweza kuwa ameathirika kiasi cha kushindwa kukaa?
Tumepanga kumpeleka kwa wanasaikolojia na watu wa therapy mara tu akimaliza mitihani yake.
Asanteni!