Msaada: Fundi kasema gari yangu ina shida ya Sensor

bhachu

JF-Expert Member
Joined
Jul 29, 2015
Posts
8,443
Reaction score
9,854
Wadau naamini JF naweza pata msaada juu ya hili suala?

Iko hivi kuna mkebe nimenunua hivi karibuni ila kuna kitu huwa nakiona kwenye dashboard huwa sikielewi, kitu chenyewe kinawaka kwa rangi ya "kijani" alafu yanatokea maandishi ya neno "ECO", kuna fundi nilimpelekea akanambia kuna shida kwenye Sensor gani sijui, akanambia kutengenezeka itahitajika laki moja na nusu, so nmeamua ni share na nyie wadau maana ni kama family kwangu.





Pia wadau nlikua naomba mnielimishe juu ya matumizi ya hiyo gia "S" n "B".

 
Hahahah mkuu fundi wako miyeyusho atakupiga hela mda si mrefu😂!

“Eco” ni kifupi cha neno Economy ama uchumi kwa maana ufanisi wa hali ya juu katika matumizi ya nishati ya mafuta katika gari yako.

Endapo hio taa itawaka basi tambua kuwa uendeshaji wako ni sahihi na unapelekea ulaji mzuri wa mafuta. Endapo utaanza kukanyaga race za ajabu ajabu zaidi ya 2.5RPM utaona hio taa inazima kuashiria uendeshaji wako ni mbovu na utachangia ulaji mbaya wa mafuta ya chombo chako.

So furahia hio alama zaidi kuliko kuwa na wasiwasi haina shida iko hapo kukupa marks za uendeshaji wako. Ikiwaka “Eco” maana yake upo on the right track ila ikizima kama ni ruti za mjini pekee jua tu utaenda sana sheli.

Kuhusu herufi “B” hio ni mahususi kwa engine braking. Unasukumia speed icontroliwe na engine kwenye miteremko
 

Daaaah shukrani sana kaka kwa elimu hii.
 
Wadau naamini JF naweza pata msaada juu ya hili suala, iko hivi kuna mkebe nmenunua hivi karibuni ila kuna kitu huwa nakiona kwenye dashboard huwa sikielewi, kitu chenyewe kinawaka...

Kwenye gari

Taa ya Kijani/Blue inaonesha taarifa.

Taa ya Njano/Orange Inaonesha Tahadhari.

Taa nyekundu hatari.

Hii ni Vitz au Belta?
 
Hahahah mkuu fundi wako miyeyusho atakupiga hela mda si mrefu😂!

“Eco” ni kifupi cha neno Economy ama uchumi kwa maana ufanisi wa hali ya juu katika matumizi ya nishati ya mafuta katika gari yako...
"S" ina maana gani pale?
 
Huyu mwamba yupo sahihi kabisa.
 
Huyu mwamba yupo sahihi kabisa.
 
Sasa huyu fundi wake angeizimaje iyo taa Kama angepewa hiyo tenda? au angekata waya [emoji23][emoji23][emoji23]
[emoji1787][emoji1787][emoji1787]
Washenzi wale wa chini ya mwembe...
Wanaizima kwa kuondoa hicho kitaa kinachowaka kwa ndani..
Au wanafungua hiyo instrument cluster, wanabandika tape nyeusi...mwanga wa kitaa hautaonekana tena...

Wanakupiga hela namna hiyo...

Hata check engine light wale wahuni wanazizima namna hiyo....utashangaa ukiweka switch on, taa ya check wngine haionekani..[emoji1787][emoji1787]
 
Pia ogopeni sana mafundi wanaowaambia..
Nielekeze kazini kwako ni wapi nije nikachukue gari, nilitengeneze ulipitie jioni..[emoji28][emoji28][emoji2960]
Utajuta
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…