Msaada gari imegoma kuwaka

Joined
Jan 6, 2018
Posts
39
Reaction score
34
Husika na kichwa cha habari gari aina ya toyota oppa d4.

Tatizo:leo kama kawaida nimeamka asubuhi nikaiwasha ikakubali baada ya hapo nikaiacha on nikaenda kufungua bonet kuangalia engine oil na mengineyo. Kuna kitambaa nilikuwa nimeshika cha kusafishia vioo lakini kwa bahati mbaya kikaingia kwenye yale mafeni yanayozunguka pale mbele:zipo mbili ila kiliingia kwenye feni moja na gari ikazima ghafra nikaswich off then nikatoa lile tambala nikajalibu kuiwasha ikakataa nikaachana nayo nikaenda job nikajua labda tatizo linaweza kuwa betri .sasa nimerudi mchana huu nimechukua na gari ya jamaa mwingine kajaribu kunibust imegoma.haitaki kupokea moto.

Nb.yale mafeni ni auto nikiwasha yalikuwa yanawaka lakini sasa hayawaki, hata honi limegoma kupiga.

Msaada wenu kabla sijapambana na fundi tatizo ni nini hasa
 
.sasa nimerudi mchana huu nimechukua na gari ya jamaa mwingine kajaribu kunibust imegoma.haitaki kupokea moto.

Nb.yale mafeni ni auto nikiwasha yalikuwa yanawaka lakini sasa hayawaki, hata honi limegoma kupiga.
Kagua fuse, ipo mojawapo imeungua, ukiondoa hiyo nakuweka nyingine gari itawaka.

Kwa kuwa hata honi haipigi, hapo nikuwa moto(umeme) haufiki kabisa, Chunguza fuse.
 
Feni haitakiwi kuzunguka ikiwa engine haipo moto. Kazi yake ni kupoza maji ya radiator yanapofika umoto fulani, ikiwa hayo maji hayakufika huo umoto basi feni haitakiwi kuzunguka. Feni nyengine huwa ni kwa ajili ya AC ila i believe unazungumzia kuhusu feni ya kupozea maji ya moto. Jaribu kusubiria gari ipate moto ule mshale wa temp ufike katikati, kisha subiria, ukiona mshare unaendelea kuvuka kati na kupata na feni haifanyi kazi, zima gari tizama fuse. Katika fuse box itakuonesha fuse ipi ipo wapi na namba nayotakiwa, kama sikosei fuse ya feni la radiator ipo obvious imeandikwa FAN, icheki kama iko powa. Kama haipo powa badilisha. Ukiona bado, mpelekee fundi akutiamie Thermostat.
 
Amesema alienda kukagua OIL wakati engine inazinguka kitu ambacho hakishauriwi.Angekuwa amefunga tai na tai ikanaswa na hizo propeller tungekuwa tunazungumza mengine
 
We ulipotelea wapi ww??
 
Kwanza: Unapima oil wakati umewasha gari? Nani alikufunfisha kufanya hayo madudu. Usirudie, ukiwasha gari oil inaanza mzunguko na hauwezi kupata kipimo sahihi...kimsingi hupati kipimo chochote.

Pili: toa maelezo zaidi, dashboard inasoma ukiweka switch on? Muhimu kujua hilo..
Kama haisomi kabisa check ignition fuse au check fundi aangalie relay. However, hilo la kugoma kupiga hata honi nalo neno...angalia taa pia haziwaki?

Ukimaliza kuchokonoa ukishindwa...nitafute, andaa makinikia moja bombadia flani na maji baridi.
 
Piga starter huku unaminya Accelerator
Alafu moja ya fuse itakuwa ime burn out
 
Dashibord imasoma mkuu na taa zinawaka zote
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…